Your are here: Home // Habari // IDRIS SULTAN ANA UTANI NA JACK WOLPER!

IDRIS SULTAN ANA UTANI NA JACK WOLPER!

Idriss Sultan

Idriss Sultan muigizaji wa filamu Swahilihood.

IDRIS Sultan muigizaji wa filamu na mchekeshaji mahiri katika masuala ya komedi ametoa kali ya mwaka pale alipojaribu kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya akimzodoa muigizaji mwenzake katika tasnia ya filamu swahilihood Jack Wolper kwa kumwambia kuwa msanii huyo wa kike kwa mwaka huu amefunga mwaka kwa kutendwa na wanaume.

Jack Wolper

Jack Wolper muigizaji wa filamu Swahilihood.

Idriss Sultan

Idris akiwa katika uchekeshaji

Idriss Sultan

Idris katika pozi lake

Idriss Sultan

Idris akicheka

“Kiukweli inatia huruma sana ninapokutana na msanii mwenzangu Jack Wolper kila anapochangua mwanaume lazima alie, kwa mwaka 2017 Wolper amekuwa na idadi kubwa ya wanaume kuliko single alizotoa Ali Kiba,”alisema Idris.

Akiongea huku akicheka msanii huyo amedai kuwa mara kadhaa Jack amekuwa akimpata mpenzi mpya anamtambulisha kwa mbwembwe lakini siku ya siku utasikia akilia kwa madai kuwa ametapeliwa na mwanaume huyo kumbe hakuwa muoaji na pengine amemchuna na kumpotezea muda wake, anamsihi awe na siri moyo wake utakuwa na amani.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook