Your are here: Home // Habari // WASTARA AMLILIA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA KWA AJILI YA MATIBABU

WASTARA AMLILIA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA KWA AJILI YA MATIBABU

Wastara Juma

Stara muigizaji wa filamu Swahilihood. akiwa kalala

MUIGIZAJI wa filamu Bongo Wastara Juma ‘Stara’ amewaandikia ujumbe viongozi wakubwa yaani akianza na Rai wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dkt. John P Magufuli na makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akiwaomba wamsaidie kupata fedha za matibabu ya uti wa mgongo ambao alikuwa akitibiwa nchini India na muda wa kurudi ni tarehe 12 February mwaka huu.

wastara Juma

Stara akiwakatika ushungi

Wastara Juma

Stara akiwa kala Hospitali picha kutoka Maktaba.

Wastara Juma

Stara msanii wa filamu Bongo

“Sina jinsi kuomba kwa mtu mwenye kugushwa na tatizo langu kwani wale ninaowadai fedha zangu hawataki nina maumivu makali sana hadi kuna wakati nazimia na fedha ninayohitaji ni dola 18,000, namba Mh. Rais makamu wa Rais Mama Suluhu na mkuu wa Mkoa Dar es salaam wanisaidie,”alisema Wastara.

“Naamini kuwa Mama Samia ni mtu mwenye upendo na huruma akipata ujumbe huu ni rahisi kunisaidia na kila mtanzania anayeguswa na tatizo langu, nimeamua kuomba nikiwa mzima kabla sijapoteza kauli,”

Msanii huyo anasema kuwa wengi hawaamini kama hana pesa hizo lakini moja ya kampuni ya simu (Jina kapuni) ya China anaidai zaidi ya Tshs. 80 milioni lakini wamemkimbia huku wadai wengine akiwa na kesi nao mahakamani, akiangalia muda wa kurejea katika Hospitali ya Sifael nchini India umekaribia hivyo ni vema kuomba msaada mwenye kuguswa amsaidie.
Stara kwa sasa anaishi katika wakati mgumu sana kwani anapata maumivu makali sana kutokana na maumivu ya mguu ambao umeanza kupasuka na kupata maumivu makali ya uti wa mgongo anasema pamoja na kuonyesha sura ya furaha lakini anahisi maumivu muda wote na kuvumilia tu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook