Your are here: Home // Habari // DKT.MWAKYEMBE ATOA HAMASA WASANII KUMSAIDIA WASTARA

DKT.MWAKYEMBE ATOA HAMASA WASANII KUMSAIDIA WASTARA

Joyce fisso, Dkt. Mwakyembe, Wastara Juma

Mh. Dkt. Mwakyembe akiongea na wastara

WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameomba wasanii na wadau wengine kumchangia msanii wa filamu Tanzania Wastara Juma ili apate fedha za matibabu ya mguu wake ambao unamsumbua kwa sasa, anaamini kwa nafasi waliyo nayo wakijiweka pamoja wanaweza kumchangia mwezao na kupata matibabu.

Joyce Fissoo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Wastara Juma

Bi. Fisssoo katibu wa Bodi ya filamu akimpatia pesa Wastara mbele ya waziri Dkt. Mwakyembe akishuhudia.

Joyce fissoo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Wastara juma

Dkt. Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Wastara nyumbani kwao Tabat senene.

Godfrey Mwingereza, Joyce fissoo, Dkt. harrison mwakyembe, Wastara juma

Katibu wa Basata Muingerea, Katiibu Bodi ya filamu Bi. Fissoo na Waziri na mh. Dkt. Mwakyembe wakiwa kwa Wastara wakimjulia hali.

“Ningeomba wasanii na wadau wengine tumchangie msanii mwezetu kwa ajili kupata matibabu ya mguu wake kwa kweli anaumwa kila mmoja wetu akitoa kile alicho nacho kitasaidia na kumuondolea maumivu Wastara,”aliasema Dkt. Mwakyemba.

Mh. Waziri alifika nyumbani kwa Wastara Tabata Sanene akiwa ameongozana na Katibu mtendeji wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo , katibu wa BASATA Godfrey Mwingireza pia waziri aliweza kumchangia fedha kiasi cha Tshs. 1,000,000 ikiwa ni hamasa kwa wasanii kuweza kumchangia msanii mwezao.

Aidha katibu mtendaji wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo amempa faraja Wastara kwa kumpongeza kwa ujasiri pia asikate tamaa aendelee na ujasiri huo Mungu atampa heri, kwani amekuwa jasiri na anaguswa na tatizo lake kwa sababu ni moja kati ya wadau wake kwa upande wa tasnia ya filamu nchini.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook