Your are here: Home // Habari // FILAMU KUBWA KUTENGENEZWA NA WANA MOROGORO WENYEWE

FILAMU KUBWA KUTENGENEZWA NA WANA MOROGORO WENYEWE

Haviti Makoti

Makoti muigizaji wa filamu Swahilihood.

Wasanii wa filamu mkoani Morogoro wakiongozwa na msanii kinara wa mkoa huo, Haviti Makoti anayefanya vizuri katika tamthilia ya Jirani inayorushwa na kituo cha ITV wanatarajia kufanya filamu kubwa mwanzoni mwa mwaka huu kwa kushirikiana wadau mbalimbali na vituo kadhaa vya redio na runinga vya Morogoro.

Ignas Mkindi

Ignas Mkindi mwandishi wa Muswada wa filamu hiyo,

Haviti Makoti

Haviti Makoti muigizaji wa filamu Swahilihoo

Filamu hiyo itakayoonyeshwa kwenye majumba mbalimbali ya sinema nchini inatarajiwa kuwashirikisha wataalamu mbalimbali wa filamu nchini ambao msemaji wa mradi huo hakuwa tayari kuwataja japo alidokeza kuwa mswada umeandikwa na mwandishi aliyebobea, Ignas Mkindi.

Akiongea na mwandishi wetu, msemaji wa mradi huo bwana Edson Magwila aliwataja baadhi ya wasanii walioko mstari wa mbele katika mradi huo unaofanyika chini ya mwamvuli wa ushirika wa Swahilifilms ni Fadhili Mbunge, Mama Daudi na Remember Msapwa.

Akifafanua zaidi kuhusu mradi huo, Magwila ameutaja mradi huo kama ni muhimu sana katika kuwatoa wasanii wa Morogoro kwenye upigaji wa filamu za gharama ndogo wanazoishia kuzunguka nazo kuuza mikononi na kuanza kufanya filamu kubwa zinazoweza kuleta ushindani kitaifa na kimataifa.

Aidha aliwaomba wadau mbalimbali waliojitokeza kusapoti mradi huu waendelee kuwa bega kwa bega katika kufanikisha mradi huu utakaoleta sura mpya katika tasnia ya filamu mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.
Attachments area

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook