Your are here: Home // Habari // KUOLEWA NA KUOA NI UFUNGWA – RAYUU

KUOLEWA NA KUOA NI UFUNGWA – RAYUU

Alice Bagenzi

Rayuu muigizaji wa filamu Swahilihood

MUIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Bongo movie Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amedai kuwa maisha ya ndoa yanahitaji umakini mkubwa sana na kabla ya mtu kuingia katika uhusiano hadi kufikia watu kuoana lazima kuwe na utulivu mkubwa sana kwani moja ya changamoto kubwa ni mama wakwe na mawifi.

Alice Bagenzi

Rayuu akiwa katika pozi la picha

Alice bagenzi

Rayuu katika pozi

“Kuolewa au kuoa ni ufungwa kuna wakati inabidi kila mtu amlinde mfungwa wake, ukichemka lolote linaweza kutokea na ndoa kuruka mbawa na kila mtu akibaki akijutia au kulia tu bila ufumbuzi wa tatizo,”alisema Rayuu.

Msanii huyu wa filamu na tamthilia wa kitambo anasema kuwa pale kila mtu anavyojua kuwa yupo katika kifungo ni wajibu wake kumlinda mfungwa wake ambaye anaweza kuwa mke au mume, kwa sababu changamoto kutoka kwa ndugu uchukua nafasi hata kama mnapendana kwa maneno ya wanandugu mnaweza kutengana.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook