Your are here: Home // Uchambuzi // FILAMU YA MWALIMU MASEMELE IMEKUJA NA UJUMBE SAFI KWA JAMII

FILAMU YA MWALIMU MASEMELE IMEKUJA NA UJUMBE SAFI KWA JAMII

Mwalimu Masemele film

Filamu ya Mwalimu Masemele kutoka bongo

FC Movie Preview kuanzia sasa itakuwa ikikuletea uchambuzi wa filamu ili kukupa nafasi kupata undani wa kazi husika kama ilivyo katika kazi yoyote inayofuata uwepo wake kwanza kabla ya kuangalia kazi yetu tutakayoipitia leo ni vema kujua hasa misingi inayojenga uwepo wa filamu kamili kitaaluma.

Maulid Ali

Mwalimu Masemele akiwa darasani na wanafunzi (Maufundi)

Maulid ali

Maufundi mtayarishaji wa filamu ya Mwalimu masemele.

Mwalimu Masemele film

filamu ya mwalimu Masemele

Sinema iliyokamilika inajengwa na vitu vitatu muhimu ambavyo ni 1. Sinema yenyewe (Cinema), 2 Watazamaji (Audiences) na tatu ni Uchambuzi (Critics) kwa kuangalia haya ndio filamu inakuwa imekamilika japo kwa hapa kwetu wengi wangependa uchambuzi uwe chanya tu kwa watengenezaji wa filamu (Filmmakers).

Nimeanza kwa kufafanua kidogo ili kila mtu anatayefuatilia makala katika site yetu aweze kusafiri nasi kwa pamoja na kushiriki kwa maoni pia kuchagua sinema ambazo ungetamani tuanze nazo katika uchambuzi wetu huku lengo kuu kusaidia ukuaji wa tasnia ya filamu Bongo.

Kama nilivyokujulisha filamu yetu ya leo ni Mwalimu Masemele ambayo imeigizwa na Maulid Ali (Maufundi), Abdalah Muki (Mwalimu Mkuu), Lamia Lulandala (Mwalimu), Monica Sizya (Likubona), na Amri Athuman ‘King Majuto’ mganga .

Mtunzi ni Maulid Ali akishirikiana na Henry Mwakajumba ambaye pia ameongoza filamu hiyo, filamu ya Mwalimu Masemele maudhui yake ni kijana ambaye anafanya kazi Gereji na kukabiriwa na maisha magumu akiishi na mkewe ambaye anampa changamoto.

Hadithi kwa ufupi Mwalimu Masemele ambaye ni kijana anayeganga njaa mtaani na kunyanyaswa na bosi wake anapata habari za wito wa kuteuliwa kuwa mwalimu kaka yake ambaye ni marehemu hivyo Masemele anafunga safari kwenda Mkoani Morogoro vijijini anakutana na changamoto nyingi njiani.

Akiwa hajafika shuleni kuripoti anakutana na vijana ambao anawajibu vibaya wanasirika na kutaka kumpiga wanamkimbiza na kuingia kujificha katika nyumba ya mganga wa jadi Mzee King Majuto akiwa hapo baada ya kupotea anatumia muda huo kuiganga.

Kijana Masemele hana fani ya ualimu wala hajawahi kusomea popote lakini kutokana na ugumu wa maisha anagushi vyetu vya marehemu kaka yake na kupokelewa katika shule husika na kuanza kazi ya ualimu kwa kuunga unga lakini anakabiriwa na upinzani kwa walimu wenye taaluma.

Hiyo ni sehemu ya filamu ya Mwalimu Masemele ambayo kiukweli maudhui yake ni jinsi gani mtu anaweza kugushi vyeti au chochote ndio tunachoona katika filamu ya Mwalimu Masemele kwa kuanza mwaka 2018 ni filamu iliyoweza kuwakilisha ujumbe halisi hasa wakati huu ambao Serikali inawafukuza wenye vyeti bandia.

Kumbe tafsiri ni kwamba ugumu wa maisha uunaweza kukufanya uvunje sheria hata kama unajua ni kosa ndio alichokifanya Maufundi kwa kwenda kufanya kazi asiyo na ujuzi nayo kwa kutumia vyeti vya marehemu kaka yake ambaye alitakiwa kwenda kufundisha katika shule husika.

Tupitie nafasi za wahusika tuone kila mtu ambavyo amejaribu kuitendea haki nafasi yake.

Wasanii (Actor & Actress)
Wasanii hasa muigizaji kinara Mwalimu Masemele (Maufundi) ameigiza kwa kiwango cha hali ya juu sana na kuifanya filamu hiyo kuwa na ubora wa kipekee anastaili hongera pamoja na washiriki wengi.

Mavazi (Costumes)
Mavazi mtu wa mavazi amefanikiwa kufanikisha kazi aliyopewa na mtayarishaji wa filamu hiyo.

Mandhari (Location)
Mtu wa mandhari amefanikiwa kufanikisha kazi yake kuanzia nyuma shule vitu vinavyowakilisha hali halisi maisha ya vijijini.

Muongozaji (Director)
Muongozaji wa filamu ameitendea haki kwa kuongoza vema anastaili pongezi.
Mpiga picha jongefu (Cinemagrapher)
Mpiga picha amefanya kazi yake kwa ufasaha na kufanikisha filamu hiyo.

Mtu wa sauti (Sound man)

Mtu wa sauti alifanya kazi yake vema hauna haja ya kukaa na Remote ili upate kazi ya kushusha na kupandisha sauti hongera.

Ujumbe wa filamu hiyo unafundisha sana na jambo la kipekee ni kutokana na wahusika kuwa ni wachekeshaji lakini wanafanikiwa kuwakilisha ujumbe unaofundisha uburudisha na kuelimisha ni wakati mzuri kwa watayarishaji wengine kujifunza na kufanya kazi nzuri zaidi. Kama walivyofanya filamu ya Mwalim Masemele.

Kwa maoni tuwasiliane
+255 624 113 968 info@filamucentral.co.tz/ eutambuzi@gmail.com

filed under: Uchambuzi

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook