Your are here: Home // Habari // MABWANA WA KIKONGO KWA KUSIFIAA – JACK WOLPER!

MABWANA WA KIKONGO KWA KUSIFIAA – JACK WOLPER!

Jack Wolper

JACK Wolper msanii wa filamu Bongo

MUIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Jaqueline Wolper ‘Jack’ anasema kuwa amewashitukia wanaume si wakuiwategeemea kwa maisha endelevu kwani unaweza kupotea ukaamini unapendwa kumbe yupo naye kikazi, hivyo akili yake anawekeza katika mambo yake ya kibiashara ni kujitaidi kuwa mbunifu .

Jack wolper

Jack Wolper muigizaji wa filamu bongo

jack Wolper

Jack katika pozi lake la picha

“Kuna wanaume wanajua kusifia hasa ukimpata mwanaume wa Kikongo unahisi dunia yote ni mali yako lakini kumbe hakuna lolote subiri sasa akuchoke unajishutukia umemaliza kila kitu yeye anakukimbia,”alisema Jack.

Pamoja na kuwa mjasiriamali msanii huyo anadai kuwa kwa sasa amejikuta akigeukia katika masuala ya ubunifu wa mavazi na kufanikiwa lakini malengo yake ni kuwa na lebo kubwa ya mavazi na bidhaa nyingine ambazo atauza popote na si ndani ya Bongo tu.

Jack anasema kuwa anapenda sana akina dada ambao wana wanaume ambao ni Wakongo kwani wanaume hao ni mabingwa wa kusifia japo si watoaji mkwanja kwa wanawake, lakini wakianza kumsifia kitu mtu lazima wanunue jambo ambalo linamnufaisha yeye kulingana na biashara yake ya nguo.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook