Your are here: Home // Habari // UJUZI WANGU UNANILINDA BONGO MOVIE – TINO

UJUZI WANGU UNANILINDA BONGO MOVIE – TINO

Hisany Muya

Tino muigizaji wa filamu Swahilihood

WASWAHILI wanasema shida mgunduzi hasa pale mtu anapoweza kuendeleza maisha yake kwa kuwa na vipaji vingi kama kwa msanii wa filamu Hisany Muya ‘Tino’ kwani anaishi kulingana na msimu au biashara gani inampatia riziki anasema msanii huyo ambaye ana vipaji kama fundi sofa, magari, umeme na uwashi.

Hisani muya

Tino akiwa katika pozi la picha

Hisany muya

Tino muigizaji wa filamu Swahilihood

“Nina vipaji lukuki lakini kazi ambayo imenipa jina na kunijenga ni sanaa ya uigizaji kutokana na ali ya filamu kutikisika kidogo nimerudi katika kazi zangu na nafanya kwa wale wateja wangu wanaonijua tu ili maisha yaende,”alisema Tino.

Tino anasema kuwa kazi zake zote hizo mara nyingi anazifanya kwa kuwafuata wanaohitaji huduma za kiufundi japo kazi kama za useremala uzifanyia kwake, hivyo anajaribu kuwashauri wasanii wenzake kama mtu ana ujuzi wa kazi nyingine zaidi ya kuigiza kutoipuuzia kwani kuna siku itamsaidia kumpatia kipato.

Aidha msanii huyo ametamba kwa kusema kuwa pamoja na ujuzi alionao kujulikana kwa wateja wengine pia wasanii wengi wamekuwa wateja wa kazi zake ikiwa kuwauzia magari kuwabunia mitindo mbalimbali katika nyumba zao kuanzia ujenzi hadi kupamba nyumba kwa rangi na mapambo mengi ndani ya nyumba, bila kuacha uigizaji wa filamu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook