Your are here: Home // Habari // MZAZI MWEZANGU ALIKATAA KUOLEWA NA MIMI- MUSA BANZI

MZAZI MWEZANGU ALIKATAA KUOLEWA NA MIMI- MUSA BANZI

mussa Banzi

Mussa Banzi akiwa katika vazi la harusi.

MUONGOZAJI na mtayarishaji mkongwe wa filamu Bongo movie Mussa Banzi amefunguka kuwa sababu ya yeye kuzaa na wasanii ni mazingira ya kikazi kwani wapo muda wote na lengo kuu ni kuwaoa lakini mara nyingi wao pengine wanamwangusha kwa kushindwa kuvumilia maisha ya ndoa na kujikuta wanaishia kuzaa naye tu.

Jennifer Ernest

Leila mke wa kwanza wa Mussa Banzi aliyetengana naye baada ya kuzaa naye watoto wawili

Mussa Banzi

Mussa Banzi katika pozi la picha

mussa banzi

Mussa Banzi muongozaji, mtuzi na mtayarishaji filamu Swahilihood.

Mariam Chobis, Mussa Banzi

Mussa Banzi akiwa na Marisa mzazi mwezake katika picha ya pamoja

“Mazingira yetu ya kikazi ndio tunatengeneza mahusiano mke wangu wa kwanza nimezaa naye watoto wawili na nilifunga naye ndoa na wa pili nilizaa naye mtoto mmoja wakati nipo katika taratibu za kuoa akakataa,”alisema Mussa Banzi.

Mzazi mwezake ambaye alifanikiwa kuzaa naye kisha kukataa kuolewa naye ni Mariam Chobis hivyo kwa sababu lengo lilikuwa ni kuoa kwa ajili ya kuwalea wanaye aliamua kuoa lakini si mwanamke ambaye si muigizaji na ndoa imedumu na anaendelea kuishi naye pengine imekuwa vigumu kuishi na wasanii katika maisha ya ndoa.

Banzi anasema kuwa kuna wakati watayarishaji wanapewa kashifa za rushwa ya ngono lakini inawezekana linaweza kuwa jambo hilo halina ukweli anafikiria sekta ya filamu ni sawa tu na fani nyingine ambazo kiongozi anaweza kuwa na mahusiano na mfanyakazi mwezake na kuoana kwa kufuata taratibu husika.

Unavyomuongelea Mussa Banzi ni mtu muhimu sana katika tasnia ya filamu kwani ndio mtunzi na mtayarishaji pekee ambaye ameweza kuibua vipaji vya wasanii wenye majina kama Riyama Ali, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Shumileta, Batuli, Mohamed Likulo ‘Dimoso’ na wengine wengi bila kupitia katika tamthilia na kuwa nyota Bongo Movie.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook