Your are here: Home // Habari // NYAMAYAO ANAIPENDA NCHI YAKE YA TANZANIA

NYAMAYAO ANAIPENDA NCHI YAKE YA TANZANIA

Happiness Stanslaus

Nyamayao muigizaji wa filamu Swahilihood.

HAPPINESS Stanilaus ‘Nyamayao’ muigizaji nyota katika tasnia ya filamu anasema kuwa kipaji chake kimemsaidia kujua mengi ya ulimwengu na kujikuta anakuwa mzalendo kwa Taifa lake la Tanzania kwa kulitangaza kwa mavazi na Lugha ya Kiswahili kwani ni bidhaa muhimu sana kwa sasa pia ni ajira kwa vijana wengi.

Hapiness Stanslaus

Nyamayao msanii wa filamu Swahilihood.

Hapiness Stanslaus

Nyamayao katika pozi la picha.

Happiness Stanlaus

Nyamayao katika pozi la picha

“Tunapokuwa nje ya Tanzania upendo unaongezeka na kupigania Taifa langu nimerudi kwa ajili ya Likizo yangu nikitokea nchini China kwa ajili ya kazi maalum ya kuingia sauti katika tamthilia na filamu kiswahili kipo juu,”alisema Nyamayao.

Nyamayao anajivunia nafasi yake ya uigizaji imepatia ajira nyingine kwa njia ya kuigiza kwa sauti tu, pia msanii huyo anasema wakiwa nje wanajitahidi sana kuvaa mavazi ya kiafrika kwa ajili ya kutangaza utamaduni wa Kitanzania kama wafanyavyo wao watu wa nchi za magharibi kulinda utamaduni wao.

Msanii huyo anapendelea kuitangaza Tanzania kwa njia ya mavazi kama vile uvaaji wa Vitenge na staili za kiafrika na kuwa tofauti na wachina wenyewe ambao wanajulikana kwa mavazi yao hivyo mtu akivaa kivingine lazima aonekane kama mgeni kutoka sehemu fulani na wanapenda nao kuvaa tofauti kwa vionjo vya kiafrika.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook