Your are here: Home // Habari // SOUDBLACK MTANZANIA NYOTA WA FILAMU CHINA

SOUDBLACK MTANZANIA NYOTA WA FILAMU CHINA

Masoud Omary

Soudblack muigizaji wa filamu wa kimataifa kutoka Bongo.

MUIGIZAJI wa filamu Masoud O.Jenga ‘Soudblack’ amefanikiwa kuwa mtanzania wa kwanza kupata kampuni ya kimataifa ya uigizaji nchini China kwa kuigiza akiwa ni mtu pekee katika kampuni ya Beljing Qianxi Culture Media Service Co. Ltd msanii huyo ameingi mkataba wa miaka sita na tayari amefanikiwa kurekodi sinema nne hadi sasa.

Masoud  Jenga

Soudblack akiwa location nchini China

Masoud Jenga

Soudblack akiwa katika pozi la picha.

Masoud Jenga

Soudblack akiwa na Bunduki katika moja ya sinema alizorekodi

Masoud Jenga

Soudblack katika ubora wake nchini China.

Akiongea na Mwanaspoti Soudblack amesema kuwa kitu anachofurahia ni kufanikiwa kuaminiwa katika kampuni yenye weledi katika masula ya filamu nchini China, kwake haikuwa nafasi rahisi sana kwani katika usaili ulishirikisha wasanii watu mbalimbali kutoka katika nchi mbalimbali za kiafrika na yeye kuibuka mtu pekee kuchukuliwa na kupata mafunzo ya uigizaji.

“Nashukru nimeshakuwa msanii nyota huku China naitangaza Tanzania kwa kipaji changu ambacho nikiwa nyumbani sikupata nafasi ya kuwa muigizaji lakini China wamenipa heshimu kutokana na muonekano wangu,”alisema Soudblack.

Soudblack anasema tayari amefanikiwa kuandika muswada wa filamu itakaoigizwa nchini Tanzania na China ikielezea urafiki wa nchi hizo mbili toka miaka ya nyuma na sasa, hivyo kuna zaidi ya wasanii 50 kutoka Bongo Movie ikiwa ni moja kati ya kampeni yake msanii huyo kuitangaza Tanzania kwani anasema China wapo juu sana katika tasnia ya filamu.

Aidha amesema kuwa aliipata nafasi hiyo akiwa nchini China katika masuala ya kibiashara hakuwa amejiandaa kuwa ipo siku atakuwa msanii mkubwa katika uigiazaji akiwa Tanzania alikuwa ana rafiki zake waigizaji lakini hali aliyokuwa akiiona kwa rafiki zake ilimkatisha tamaa kuingia katika tasnia hiyo akiwa Bongo.

Soudblack ni msanii pekee kutoka Afrika ambaye ni nyota katika tasnia ya filamu nchini China baada ya kuonyesha kipaji chake cha uigizaji na kukubalika na watayarishaji wa filamu wa China na ana shauku ya kuitambulisha sanaa ya filamu Duniani ndio maana anatarajia kuja Bongo kutengeneza filamu ya China na Tanzania.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook