Your are here: Home // Habari // TUMEUA FILAMU ZETU TUTAIWEZA TAMTHILIA? – KITALE

TUMEUA FILAMU ZETU TUTAIWEZA TAMTHILIA? – KITALE

Mussa Kitale

Kitale Mkude simba muigizaji wa filamu Swahilihood.

MUIGIZAJI na mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Mussa Kitale ‘Mkude Simba’ amefunguka kwa kusema kuwa soko la Bongo movie lilikuwa juu sana lakini hivi karibuni imetokea songombingo soko la filamu kushuka na wasanii, kukimbilia kuigiza tamthilia badala ya filamu kwani soko limekwama na kusuasua.

Mussa kitale

Kitale muigizaji wa filamu Swahilihood

Mussa Kitale

Kitale akiwa katika pozi

Daud Michael, Rammy Galis

Wasanii wa filamu Bongo wanaotamba katika tamthilia nyingi Bongo

“Biashara kubwa ilikuwa katika Bongo movie lakini kwa baadhi ya wasanii wameyumba muokozi wetu labda kwa sasa ni pale wengi wa wasanii wamegeukia kwenye tamthilia, baada ya kuua filamu je na huku nako?,”alisema mkude Simba.

Msanii huyo anasema kuwa kama filamu ambayo uanzia dakika 60 tu wameikwamisha itawezekana kwa tamthilia ambayo utumia muda mrefu katika kuruka na kama tamthilia nayo itakufa kimbilio la wasanii hawa itakuwa ni kitu gani? Hivyo anajaribu kuwashauri waliokimbilia kwenye tamthilia wailinde idumu kwa maslahi ya kizazi kijacho.

Mkude Simba anatamba na filamu ya Chizi karogwa tena, Shobo Dundo na filamu nyinginezo ambazo anasambaza yeye mwenyewe bila kumpa msambazaji yoyote ikiwa ni sehemu ya kulinda haki yake ili asikose hakimiliki na haki shiriki katika kazi anazozalisha mwenyewe.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook