Your are here: Home // Habari // UZALENDO SI KUVAA TU VITO NA MAVAZI- GABO

UZALENDO SI KUVAA TU VITO NA MAVAZI- GABO

Salim Ahmed

Gabo Zigamba muigizaji wa filamu Swahilihood.

MUIGIZAJI nyota Bongo Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ anaongelea Uzalendo haujengwi kwa mavazi na vito vya thamani na kuna wakati waafrika wanaamini kuwa wapo Huru lakini inasikitisha wale walio wengi hawajui maana hasa ya uzalendo wakiamini kuwa uzalendo utajengwa kwa misemo na harakati za kuzunguka kwa kutengeneza fedha.

Salim Ahmed

Gabo Zigamba akiwa na jamii ya kimasai

Salim Ahmed

Gabo Zigamba akiwa Umasaini katika vazi maridadi la Kiasili

Salim Ahmed

Gabo Zigamba muigizaji mahiri wa filamu Swahilihood.

“Wengi hawajui faida na thamani yake na wapo tayari kurudi utumwani kwa mavazi na vito vya thamani, thamani ya mtu ni Utu na si mavazi kwani waliovaa suti ndio walioamuru wenzao wanyongwe na kusalitiwa kwa kuwafurahisha Mabwanyenye,”alisema Gabo.

Gabo anaamini kuwa Uzalendo ni kurudi katika mila na desturi zetu kwani kuna yale malezi ya kijamii yanapuuzwa na kukumbatia tamaduni za kimagharibi, jambo linaloyumbisha misingi ya Tamaduni zetu na kuingia katika mila za watu wengine na kupuuza mila zetu zile za vizazi vya watu wa kale ambao walikuwa na mawasiliano yenye faida.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook