Your are here: Home // Habari // NAPIGA MSAMBA NIIGIZE NA ANGELINA JOLIE – EBITOKE

NAPIGA MSAMBA NIIGIZE NA ANGELINA JOLIE – EBITOKE

Anastanzia Exavery

Ebitoke mchekeshaji wa Komedi Swahilihood.

KOMEDIANI wa kike Bongo movie Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ amefunguka kwa kusema kuwa kila kunapokucha anaiangalia sana sanaa anayoifanya na kujaribu kuifanya impe maslahi zaidi kwa kuishi hivyo ameamua kuanza mazoezi zaidi ya viungo na mwili kwa ujumla wake akiwa na na ndoto za kuigiza na muigizaji Angelina Jolie wa Marekani.

Anastanzia Exavery

Ebitoke katika ubora wake

Anastanzia Exavery

Ebitoke muigizaji wa filamu kutoka Bongo.

“Kila msanii jinsi anavyosonga mbele katika mafanikio yake kiusanii anatamani kufanya makubwa zaidi mimi ni mmoja wao ninafanya mazoezi ya msamba ili hata siku nitakapokutana na Angelina Jolie niwe fiti,”alisema Ebitoke.

Ebitoke anasema kuwa ana uchu sana na kufika mbali na kuwa mmoja kati ya waigizaji wakubwa duniani, anatamani awe kama msanii mkubwa Angelina Jolie kutoka Hollywood nchini Marekani, ni muigizaji ambaye anampenda zaidi pamoja na kuwa kuna wasanii kama Queen Latifa ambao ni wachekeshaji yeye ni kipenzi cha Angelina.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook