Your are here: Home // Habari // TUNAHITAJI KIZAZI KIPYA BONGO MOVIE- STEVE NYERERE

TUNAHITAJI KIZAZI KIPYA BONGO MOVIE- STEVE NYERERE

Steven Mengele

Steve Nyerere mwenyekiti wa Bongo Movie mstaafu

STEVEN Mengele ‘Steve Nyerere’ ameibua mjadala mpya baada ya kusema kuwa tasnia ya Bongo movie imeingia katika changamoto ya kudorora kutokana na wasanii kuwa wale wale kila siku na kuwazuia wasanii chipukizi kuingia katika na kupewa nafasi kama waigizaji wanaofanya vizuri katika ukuaji wa tasnia hiyo.

Steven nyerere

Steve Nyerere mwenyekiti mstaafu wa Bongo movie

Steven Mengele

Steve Nyerere mchekeshaji na muigizaji wa filamu Swahilihood.

“Kila unapoangalia filamu zetu kila siku ni sura zile zile story zinajirudia watazamaji wamechoka kuangalia sinema zisozo na ubunifu hata mimi mwenyewe nimezichoka sasa iwe kwa mtazamaji mwingine ataweza,”

Msanii huyo anasema kuwa ni wakati wa wasanii wale ambao wanaamini kuwa bila wao filamu haiwezi kufanikiwa wabadilike na kuwaachia kizazi kipya kilete mabadiliko kwenye tasnia ya filamu kwani hata wasanii wa Bongofleva wanaofanya vizuri si wale wakongwe hivyo anaamini kuwa filamu itarudi kama muziki ulivyowatoa akina Diamond.

Steve Nyerere ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Bongo Movie unity anasema kuwa changamoto iliyopo ni kubwa sana kwa waigizaji wa filamu Bongo kushindana na kazi kutoka nje kwa sababu filamu za nje zinauzwa kwa bei nafuu na zina ubora mkubwa kuliko zetu za mitaji midogo kulingana na sinema kubwa za nje.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook