Your are here: Home // Habari // NILIIKOSA SUTI YA MJENGONI KIDOGO SANA- KINGWENDU

NILIIKOSA SUTI YA MJENGONI KIDOGO SANA- KINGWENDU

Rashid Mwishehe

Kingwendu muigizaji wa filamu Swahilihood.

MCHEKESHAJI Komedi Bongo Rashid M Mzange ‘Kingwendu’ ametoa kali ya mwaka pale aliposema kuwa mwaka 2015 aliingia kugombea Ubunge huku hamu yake kuu akitamani sana kuvaa suti na Tai kama mheshimiwa Mbunge, lakini anasema hajakata tamaa anjipanga tena uchaguzi ujao mwaka 2020 ataingia katika kinyang’anyiro.

Rashid Mwishehe

Kingwendu katika pozi la kichwa

Rashid Mwishehe

Kingwendu mchekesha wa Komedi Swahilihood

“Mwaka ule nilipogombea Ubunge ilikuwa kidogo tu nichukue Jimbo la Kisarawe mimi si mtu wa watu na nilikuwa nimejipanga kwenda Mjengoni nikiwa na suti safi maana suti inapendeza ukiwa mheshimiwa ya harusi si kila mtu anavaa tu?,”alisema Kingwendu.

Kingwendu ambaye muda wote anapenda kuongea kwa kuchekesha anasema kuwa rafiki zake ndio waliomtia ushawishi kugombea na kujiona anafaa na angeweza kutetea maslahi ya ndugu zake na watanzania wote akiwa ndani ya suti ya kipekee, lakini hakusema hiyo suti ambayo alipanga kuivaa angeitoa wapi ili iwe tofauti na zingine.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook