Your are here: Home // Habari // SOKO LA FILAMU BONGO NI PRESURE- ZERISH

SOKO LA FILAMU BONGO NI PRESURE- ZERISH

Helena Luanda

Zerish muigizaji wa filamu Tanzania

MUIGIZAJI wa filamu Bongo Hellen Luanda ‘Zerish’ anadai kuwa msanii akiigiza tu si rahisi kujipatia maslahi hivyo ni kujiingiza katika utayarishaji wa filamu hapo ndio msanii anaweza kupata maslahi zaidi lakini kufanya hivyo kuna changamoto kubwa kwani baadhi ya wasambazaji ni wasumbufu ambao wanafanya kazi nje ya makubaliano.

Helena Luanda

Zerish akiwa katika pozi la picha

Helena Luanda

Zerish katika pozi lake

“Soko la filamu kwa sasa Bongo ni presure kweli unaweza hata kuzimia au kufa kabisa kama hauna ujasiri kwani unampatia kazi yako msambazaji anaisambaza katika runinga hata bila kukushirikisha na pesa hakupi,”alisema Zerish.

Msanii huyo anasema kuwa mara nyingi mawakala wa usambazaji wa filamu kwenye televisheni wamekuwa walaghai hivyo kujikuta watayarishaji wakishindwa kulipwa fedha zao kulingana na mapatano ya awali kama walivyokubaliana kwanza wanapeka kazi hizo bila taarifa zikiruka wanalipa kwa kujipangia malipo.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook