Your are here: Home // Habari // ANAYEUA FILAMU BONGO NI NANI? TOKA 40M HADI LAKI ..KADHAA?!

ANAYEUA FILAMU BONGO NI NANI? TOKA 40M HADI LAKI ..KADHAA?!

Uncle JJ film

Filamu ya Uncle JJ ya Kanumba

KILA siku zinavyosonga hali ya soko la filamu Bongo linazidi kuwa tete hakuna matumaini tena waliobaki kupigania soko hilo ni wasanii wa komedi na moja ya sababu kuu ni kutokana na kuuza kazi zao kwa bei ya chini na si kwa gharama nafuu, wale wasambazaji wakubwa hawachukui tena filamu kwani usambazaji wake umekwama.

Chanuo Film

Filamu ya Chanuo kutoka kwa Madebe Lidai

uncle jj film

Filamu ya Uncle JJ wakati huo filamu zikiunzwa kama bidhaa bora kabisa

Songombingo

Filamu ya songombingo ya Komedi kwa mfumo wao

Steven Kanumba

Marehema Kanumba enzi za Uhai wake mashabiki wa filamu wanamkumnbuka kwa kazi zake

Eti kwa sasa msambazaji kuuza nakala 2,000 ni ushindi inashangaza sana Taifa la watu milioni 50 na kuendelea kushindwa kuuza hata nakala lakini 2 kwa watu hao wote? Bado inashangaza yale maduka yaliyo kuwa yakiuza filamu za Kibongo yote yamegeuzwa na kuwa ya sinema za kizungu na tamathilia za kifilipino, sehemu muhimu kwa kuuza sinema Kariakoo kila siku maduka mapya yafunguliwa.

Kwa bahati mbaya maduka hayo ni kwa ajili ya kuuza filamu za kutoka nje ambazo hazilipii kodi yoyote na hawa ndio washindani wakubwa wa kazi za ndani ambazo wauzaji wanalalamika kama zina matozo lukuki bila kuwa na msaada wowote kwao katuika kulinda soko la filamu, wale wenye mitaji midogo wameamua kugeukia kazi za nje je tusipolipa kodi uchumi wetu utakuwa?

Maswali ni mengi sana lakini kwa sehemu ya kwanza kuhusu soko letu la filamu sitouliza mswali hayo kwani sioni wa kujibu ambapo hata ukikutana na wenye uwezo wa kujibu watakwambia kuwa kanuni na tunasubiria Sera ya Filamu kwanza ili tufanye kazi, lakini tunaona wavuvi wakinyooshwa bila kusubiri Sera ya Uvuvi.

MASLAHI KWA WASANII
Filamu ilikuwa kila siku ikipanda katika manunuzi kwa wale wenye filamu nzuri walishafika kuuza filamu milioni 40 hadi milioni 50 kutoka bei hadi leo hii kuuzwa filamu milioni 3? Hapa lazima uone Komedi zikishamiri sokoni huku zikiwa na ubora hafifi, kwani Bajeti zake ni ndogo na hata kama utakutana na filamu nzuri ambayo inauza vizuri basi ongea na wasanii wamelipwaje?

Jibu lake litakuwa sisi ni wasanii underground tumeambiwa tutafute majina kwanza kabla ya kukimbilia malipo makubwa kwa sasa je huku ndio kusema tasnia imekua kwa kiwango kipi? Hajkuna anaona kilio cha wasanii wetu na watayarishaji kutokana na kudorora kwa tasnia ya filamu Swahilihood kwani uenda hakuna taarifa sahihi kwa wenye maamuzi.

Kama mtayarishaji atajaza Makomediani kwa kila komedi yake nay eye akalipwa kwa gharama ya Tshs. 600,000 hadi milioni 1 je anawalipa kiasi gani na production analipa kiasi gani? Huku ndio mwanzo wa kurudi nyuma kisanaa kazi inapokosa Bajeti ya kutosha lazima ubabaishaji na dhuluma vitawale.
Maslahi kwa wasanii kwa sasa ni mabaya au tuseme kuwa hakuna kipato nao wamekuwa kama wasanii wa Bongo fleva hawapati pesa hadi show za matamasha huku nako Mungu si Athumani siku hizi kuna tamthilia ambazo malipo si nufaika kwa wote kama katika filamu, lakini hatuna budi kushiriki kwani bila hivyo hali ni tete majumba tuliyokodi tutashindwa kuyalipia ni heri kujisalimisha kwa wakenya.
Usikose wiki ijayo inaendelea….

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook