Your are here: Home // Habari // UBINAFSI UMEUA TASNIA YA FILAMU BONGO – KEMMY

UBINAFSI UMEUA TASNIA YA FILAMU BONGO – KEMMY

Julieth Samson

Kemmy mwigizaji wa filamu Swahilihood

MUIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya Bongo Julieth Samson ‘Kemmy’ amefunguka kuwa sababu kubwa ambayo inaifanya tasnia ya filamu kudorora na kushuka ni ubabaishaji uliyoizuguka tasnia hiyo, akianza na wasanii wakitawaliwa na ubinafsi na pia mfumo mbaya wa usambazaji.

Julieth Samson

Kemmy akiwa katika pozi la shughuli Mlimani city

Julieth Samson

Kemmy mwigizaji mkongwe bongo

“Ubinafsi kutoka kwa wasanii nacho ni chanzo kikubwa cha kufa kwa tasnia ya filamu nchini, msanii mwezako akitangulia kwa msambazaji kwako si rahisi tena kusambaza kazi yako, hatupendani na tunaogopana,”alisema Kemmy.

Pia Kemmy anasema kuwa kushindwa kuheshimu taaluma na kuweka mgawanyiko wa kazi kwa wahusika ni changamoto nyingine hivyo anawashauri wasanii wenzake wajenge tabia ya upendo na kupeana nafasi pale anapoona fursa kwa msanii mwenzake.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook