Your are here: Home // Habari // NILICHEMKA KUPUNGUA KWA KUNYWA MAJI- JB

NILICHEMKA KUPUNGUA KWA KUNYWA MAJI- JB

Jacob stephen

Jb Mtayarishaji na mwigizaji katika tasnia ya filamu Swahilihood.

MWIGIZAJI mkongwe wa filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’ amesema kuwa ushauri aliopewa na watu kuwa anywe maji apungue mwili wake ulimtesa sana lakini hakufanikiwa kupunguza unene zaidi ya kuongeza uzito na kubaki kama alivyokuwa awali, msanii aliamua kupungua kwa ajili ya filamu.

Jacob Stephen

JB akiwa mwenye sura ya furaha

Jacob Stephen

JB akiwa na john Kallaghe wakijadili jambo

“Nilikunywa sana maji hadi kusikia kizunguzungu lakini wapi bwana, kuna sinema ambayo inanitaka niwe na mwili mdogo lakini pamoja na kujibana kula mwili uligoma na kuhangaika,”alisema JB.

Jb anasema kuwa wakati akiendelea na mazoezi na kutafuta njia ambayo ingekuwa sahihi na rahisi kwa yeye kupungua ndipo alipokutana na msanii mwezake Mjomba Fujo ambaye alikuwa mnene na kumuona akiwa amepungua na kumuuliza naye alimweleza kuachana na vyakula vya wanga na sukari ndani wiki moja kapungua kilo nane.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook