Your are here: Home // Habari // BONGO MOVIE HONGERA KWA KUZIKANA

BONGO MOVIE HONGERA KWA KUZIKANA

Michael Sangu

Wasanii wa filamu wakiwa katika moja ya mazishi ya msanii

WAKATI mjadala ukiendelea ilikuwaje hadi mwigizaji mkongwe Bongo Amri Athuman ‘King Majuto’ iweje msanii huyo mwenye jina hana pesa za kujitibia hadi Mh. Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo kufunguka kuwa imebidi atoe mshahara wake kusaidia.

Michael Sangu,Hisani Muya

Wasanii wakiwa wamabeba Jeneza la msanii

Cathy Rupia, Husna

Wasanii wakiomboleza msibani Ketty , husna

Blandina Chagula, Mayasa Mrisho

Maya akiwa na Johari wakilia kwa uchungu

Michael Sangu, Suleiman Barafu

Wasanii wa Bongo movie wakiwa wanasindikiza gari

Utafiti unaonyesha kuwa moja ya tukio ambalo kama wasanii wa Bongo movie wakiamua kulifanikisha ni suala la mazishi endapo itatokea mmoja wao kufariki na kuzikwa hapa jijini Dar basi msiba utakuwa wa kihistoria na kuachana gumzo.

Hayo yametokea kwa wasanii waliotangulia mbele za haki kama Steven Kanumba, Rachel Haule, Juma Kilowoko, john Maganga na marehemu Adam kuambiana waliagwa katika viwanja vya Leaders Club na kutikisa walale mahali pema peponi.

Pamoja na hayo bado kumekuwa na changamoto pale msanii ikitokea anaugua juhudi hizi kidogo ufifia na kujikuta kila mtu anakuwa bize na kutegemea juhudi binafsi kutoka kwa wadau wa tasnia na hili limejitokeza kwa mzee wetu King Majuto.

Kwa mara ya kwanza malalamiko yametoka kuwa wasanii walijitokeza kwa ajili ya kujipiga picha kwa ajili ya kuposti katika mitandao ya kijamii kutoa lawama au kuonekana walifika kumjulia hali, lakini kutokana na hali ngumu ya kiuchumi hakuna mwenye uwezo kuchangia.

Bongo movie pia wamepewa hongera kwa kuwa ni sehemu ya kufanikisha mazishi ya Video Queen Masogange kwani inawezekana ikiwa amefunika hata baadhi ya misiba ya waigizaji walitutoka kwa watu kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo.

Masogange alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar na mwili wake kuagwa Aprili 22 katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni na kusafirishwa nyumbani kwao Mbeya kwa mazishi yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.

Pengine ni wakati wa kuangalia njia nyingine kwa wasanii wa filamu kukumbuka katika pesa kiduchu inayopatikana kukata Bima ya Afya kwani inaonekana inaweza kumsaidia endapo msanii atapata maradhi kwani pamoja na umaarufu na kuonekana kama ni watu wenye pesa hali ni tofauti.

Mwisho ningependa kuwashauri wasanii wawe kama vile wasanii wa Bongo fleva ambao tunasikia wana mameneja japo sifahamu mikataba yao kama wanafanya kazi husika kwa ajili ya kusimamia kazi zao na kuuza kwa maslahi zaidi ili kuepuka kipengele cha msaada wa kupitiwa mikataba upya.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook