Your are here: Home // Habari // SIJAHAMA BONGO KENYA THEN HOLLYWOOD– DUMA

SIJAHAMA BONGO KENYA THEN HOLLYWOOD– DUMA

Daud Michael

Duma mwigizaqji wa filamu Swahilihood

MSANII wa filamu Bongo Daud Michael ‘Duma’ amesema kuwa hajakimbia Bongo na kuhamia nchini Kenya kama baadhi ya watu wanavyozusha bali yupo nchini Kenya kikazi na atakapomaliza kazi yake ya kisanaa atarudi nchini na kuunga na wasanii wenzake katika shughuli zake za uigizaji anaofanya Kenya.

Daud michael

Duma akiwa katika pozi la picha.

Daud micahel

Duma msanii wa filamu Bongo

Daud michael

Duma akiwa katika moja ya scene za tamthilia ya Nyota nchini Kenya.

“Siwezi kuhama Bongo wala kuikimbia hapa ni kwangu ni suala la utafutaji na kwa sasa mimi ndio msanii wa kimataifa nipo Nyeri nchini kenya nikirekodi tamthilia ambayo pia uruka Bongo ya Nyota so nipo kikazi zaidi,”alisema Duma.

Duma anasema alipoitwa na mtayarishaji wa tamthilia hiyo alikubalia haraka kwani lengo lake ni kwenda kuigiza Hollywood kufanya kazi na watu wa Kenya ni rahisi kumuunganisha hata na msanii mkubwa kama Lupita Nyongo muigizaji mkubwa kutoka Afrika ya Mashariki ambaye yupo katika filamu maarufu ya Black panther.

Msanii huyo anasema anapenda changamoto katika kazi ndio maana anafanya kazi na wasanii wa kimataifa huku lengo lake kuifunika Afrika ya Mashariki kwani hadi sasa anayemuumiza kichwa ni msanii wa kimataifa anayeigiza Hollywood Lupita Nyongo ambaye ni mwigizaji bora wa kike tuzo za Oscar kupitia filamu ya Slave.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook