Your are here: Home // Habari // ISHU YA KING MAJUTO HURUMA KWA WASANII WOTE

ISHU YA KING MAJUTO HURUMA KWA WASANII WOTE

Amri Athumani

King majuto mwigizaji wa filamu Swahilihood

IPO imani kuwa ilimpasa Bwana Yesu ateswe ili Dunia ipate kuokolewa hivi karibuni mjadala mkubwa uliibuka Bungeni wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo waziri husika akiongelea suala la kuugua msanii Amri Athumani ‘King Majuto’.

Ummy Mwalim , Amri Athuman

Waziri wa Afya Ummy Mwalim akiwa amemtembelea King Majuto kumjulia hali

Dr. Harrison Mwakyembe, Amri Athuman

Dr. Harrison Mwakyembe akiwa na King Majuto Hospitali ya Taifa Muhimbili akifurahia jambo

Amri Athumani

King Majuto mwigizaji wa filamu Swahilihood.

Amri Athuman, Dr. Harrison Mwakyembe, Hamza Athuman

King Majuto akiwa na mtoto wake Hamza Athuman na Dr. Harrison Mwakyembe

Mjadala huo unakuja baada ya kuhitaji fedha kwenda kutibiwa nje ya nchi baada ya kusumbuliwa hapo awali na tezi dume lakini sasa akisumbuliwa na nyonga ambayo inamfanya atembelee magongo, Dr. Mwakyembe anatangaza vita na wale wote wanaotumia wasanii kwa mikataba mibovu.

Mh. Waziri analalamikia mikataba mibovu yenye ulaghai hivyo wasanii wadogo wanahisi uenda kupitia King Majuto ndio mwanzo wa kupata haki zao, wengi wanashangaa kwa umahiri msanii kama Majuto kukosa pesa ya matibabu je kwa wale wasio na majina kama yeye itakuwaje?

“Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana wasanii wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa-empower (kuwawezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wasitumie middle men,”

“Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu, maisha yenyewe unayaelewa waheshimiwa.. lakini nusu ya mabango ya biashara ni ya Mzee Majuto.“

Waziri ameunda Kamati ya wanasheria, itaanza na kesi ya Mzee Majuto, kwa kupitia mikataba ya Mashirika yote na makampuni yaliyoingia mikataba na Mzee Majuto kuiangalia upya mikataba hiyo, kama alionewa ni lazima ilipwe familia yake, baadaye kwa Kanumba na msanii yeyote ambaye anaona aliingia mkataba wa wenye mashaka.

Hivyo wasanii wanatakiwa kujitokeza kusaidiwa kupitiwa mikataba yao yenye ubabaishaji, tayari King Majuto anaelekea kutibiwa nchini India kwa matibabu baada ya kupata msaada Serikalini na wadau waliomchangia kufanikisha matibabu yake msanii alikuwa amelazwa wodi ya Sewahaji namba 18 sehemu ya Private.

Pamoja na hayo wachunguzi wa mambo wanashitushwa na mpango huo kwani tatizo ni mfumo na si wasanii kudhulumiwa wadau wa tasnia ya filamu wanalalamika kuzorota kwa soko ambalo limebanwa na kazi za nje matozo mengi sana kuliko ukusanyaji.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook