Your are here: Home // Habari // NAIGIZA SITAKU KUWA OMBAOMBA- MAMA KANUMBA

NAIGIZA SITAKU KUWA OMBAOMBA- MAMA KANUMBA

Frorence Mtegoa

Mama Kanumba mwigizaji wa filamu Swahilihood

FLORENCE Mtegoa mama wa mwigizaji nyota Bongo marehemu Steven Kanumba amefunguka kwa kusema kuwa anashangaa baadhi ya watu kumjadili kuwa kwanini anaigiza, lakini hawaongelei uwezo wake na kipaji chake alichopewa na Mungu wanabaki kushangaa kwanini anaigiza.

Florence Mtegoa

Mama Kanumba katika pozi

florence Mtegoa , Ramsey Noah

Mama Kanumba akiwa na mwigizaji wa kimataifa kutoka Naijeria Ramsey Noah

“Ujue masuala ya sanaa ni ndani ya damu ya mtu lakini pia ni kazi kama kazi nyingine, mimi naigiza kwa ajili ya kuendesha maisha yangu na si kwa ajili ya kuuza sura vijana wasemavyo kama alivyokuwa mwanangu,”

Aidha mama Kanumba anasema kuwa anajituma katika kuigiza kwani siku za nyuma mwanaye ndio alikuwa mlezi wake na sasa hayupo tena hawezi kuwa omba omba ni bora atumie kipaji alicho nacho cha kuigiza kuliko kutegemea fedha za kuomba.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook