Your are here: Home // Habari // DODOMA ARTS CENTER MKOMBOZI WA WASANII WA FILAMU BONGO

DODOMA ARTS CENTER MKOMBOZI WA WASANII WA FILAMU BONGO

Abdalah Mkumbila, Grevas Kasiga, deo

Muhogo Mchungu akiwa wahitimu wa Mafunzo

MWANZA WALAMBA DUME
BAHATI kubwa kwa mwaka huu iliwaangukia wasanii wa Jijini Mwanza pale Dodoma Arts Center walivyojitoa kwa ajili ya kujenga weledi kwa waigizaji wa filamu Bongo, semina ya kwanza kubwa imeangukia kwa wanamwanza mafunzo haya ni chini ya Mkufunzi Grevas Kasiga (Chuma).

Grevas Kasiga

Chuma akiwa na wahitimu wa mafunzo Jijini Mwanza

Abdalah mkumbila, Grevas Kasiga, Deo

Chuma , Deo na Muhogo Mchungu wahitimu wa mafunzo ya filamu

Grevas kasiga, Deo

Baada ya mafunzo nadharia wahitimu na wakufunzi kwa vitendo sasa, wakitayarisha filamu ya Majuto

Abdalah mkumbila , Grevas Kasiga, Deo

Wakufunzi wakiwa katika mafunzo ya vitendo wakitengeneza filamu fupi ya Majuto

Mafunzo yalianza tarehe 16/04/2018 mpaka tarehe 30/04/2018 mafunzo hayo yalihusu utayarishaji wa filamu kupitia Taasisi ya Dodoma Arts Center jijini Mwanza. Chanzo cha kufanya mafunzo haya ilikuwa ni kuinua Ubunifu na soko la utayarishaji filamu nchini Tanzania.

“Tulifanya utafiti na matokeo ya utafiti huo yaligundua kuwa kuna sababu kadhaa ambazo zimechangia kushuka au kuanguka kwa soko la filamu za Kiswahili nchini Tanzania. Moja kati ya sababu za msingi tuliona ni kushuka kwa kiwango cha ubunifu katika filamu zetu,”alisema Kasiga

Mkufunzi huyo amedai kuwa watayarishaji na watengeneza filamu hapa nchini wamekuwa wakitayarisha filamu kwa mazoea huku wakisahau kuwa watazamaji wetu wamekuwa wakikua kiutazamaji kutokana na maendeleo ya kimawasiliano na utandawazi kwa upana wake.

“Watazamaji wetu wamekuwa “exposed” na uangaliaji wa filamu kutoka tasnia kubwa za kidunia kama vile Hollywood, Bollywood, Korea movies, Chines movies, Ufilipino na kadhalika,”

Hilo limewafanya wawe mbele kwenye kuona vitu vizuri ambavyo wanategemea kuviona katika filamu zetu lakini hawavioni na hivyo kuanza kuchagua filamu chache za kitanzania za kuzitizama. Hivyo katika kuinua soko na ubunifu wake, wameanza kwa kutoa elimu kuhusu utayarishaji wa filamu katika maeneo yote makuu kuanzia ubunifu katika Uandishi wa miswada (scripts).

Uigizaji wa kifilamu, mbinu za uchukuaji wa picha jongefu (Film Production) pamoja na Uongozaji filamu, katika darasa hili waliona ni vema kuanzia Mwanza kutokana na kuwa ni kitovu cha soko linalouza zaidi katika filamu za kitanzania na pia kuinua tasnia kwa kuwa na viwanda vidogo vidogo vya utayarishaji wa filamu nchini vitakavyokwenda kujenga tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa kiwango kipana.

Hili pia kwetu limekuwa liko sambamba na sera ya nchi ya kuinua viwanda kwani tunaamini tasnia ya filamu nchini Tanzania ni kiwanda kikubwa cha ubunifu kinachoajiri idadi kubwa ya watu katika muktdha wa kisanaa na kwa watendaji wengine wanaosaidia biashara hii ya filamu.

Katika mafunzo yetu ya wiki mbili ya Jijini Mwanza waliweza kutayarisha filamu fupi inayoitwa “Majuto” yenye lengo la kushajiisha vijana kujali afya zao ili kuondokana na magonjwa ya maambukizi kama UKIMWI na kuongeza nguvu kazi katika jamii, ikiwa ni mafanikio ya mafunzo hayo kupima uelewa wa wahitimu.

Wakufunzi katika mafunzo haya walikuwa ni: Abdallah Mkumbullah (Muhogo Mchungu) ambaye ni muigizaji nguli hapa nchini, Deo Surah ambaye ni Mkufunzi wa masuala ya Midia kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania na Gervas Kasiga (Chuma/Junior wa Kaole Sanaa group) ambaye ni Mhadhiri wa Fasihi na Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Tanzania.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook