Your are here: Home // Habari // TABIA NJEMA YA LULU ANUFAIKA NA KIFUNGO CHA NJE

TABIA NJEMA YA LULU ANUFAIKA NA KIFUNGO CHA NJE

Elizabeth Michael

Lulu mwigizaji wa filamu Swahilihood

MWIGIZAJI wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amebadilishiwa kifungo na sasa atatumikia kifungo nje ya Gereza huku akifanya kazi za kijamii, Lulu anakuwa katika kundi lillonufaika na msamaha wa Mh. Rais Dkt. John P. Magufuli uliotolewa tarehe 26. April. 2018 siku ya Muungano.

Magereza Lulu

Taarifa ya kubadilishiwa kifungo Lulu kutoka magereza

Elizabeth michael

Lulu mwigizaji wa filamu Swahilihood.

Elizabeth Michael

Lulu akiwa katika pozi la picha

“Mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameachiliwa leo tarehe 12. May. 2018 kwenda kutumikia kifungo cha nje (Community Service) kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania – Dar es salaam,”Taarifa kitengo cha Habari na Uhusiano.

Kwa mujibu wa kifungi Na. 3(2)(a) cha sheria ya Huduma kwa jamiiya mwaka 2002 wafungwa ambao vifungo vyao havizidi miaka mitatu hunufaika na utaraibu huu ambao unampa fursa mfungwa kutumikia kifungo chake nje ya Gereza kwa kufanya shughuli/kazi zisizo na malipo kwa manufaa ya Jamii.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook