Your are here: Home // Habari // SITAKI KUAMINI KILA MTU NI MCHEKESHAJI- MAUFUNDI

SITAKI KUAMINI KILA MTU NI MCHEKESHAJI- MAUFUNDI

Maulid Ali

Maufundi mwigizaji wa filamu Swahilihood.

MAULID Ali ‘Maufundi’ mchekeshaji wa komedi Bongo amefunguka kwa kusema kuwa si kila mtu ana kipaji cha kuchekesha ni kazi ngumu ambayo inahitaji ukomavu, kuna wakati mchekeshaji anaweza kupanda jukwaani kuchekesha watu wasicheke.

Maulid Ali

Maufundi mchekeshaji

Maulid Ali

Maufundi akiwa katika pozi

Maulid Ali

Maufundi akiwa katika pozi la picha

“Kulingana na hali ya soko kwa sasa filamu (Dvd) hazilipi sababu filamu za kizungu ilitakiwa tuigize katika majukwaa lakini kuchekesha watu si mchezo unaweza kuona watu wanacheka kumbe wanakucheka,”alisema Maufundi.

Maufundi anasema kuwa hiyo pengine ndio sababu inayowakosesha wachekeshaji wa kitanzania kuchekesha jukwaani (Stand up Comedy) pia msanii anasema hata utamaduni wa Watanzania kuingia kwa ajili ya maonyesho ya moja kwa moja jukwaani tofauti na siku za nyuma.

Msanii huyo mahiri katika uchekeshaji hivi karibuni ameeachia wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la Moyo wangu baada ya wimbo wake Kamari ambao unafanya vizuri katika vipindi vya redio na Televisheni.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook