Your are here: Home // Habari // TUACHE LAWAMA BILA VITENDO ULITOA NINI MSIBANI? – AUNT EZEKIEL

TUACHE LAWAMA BILA VITENDO ULITOA NINI MSIBANI? – AUNT EZEKIEL

Aunty Ezejiel

Aunty Ezekiel mwigizaji wa filamu Swahilihood.

Mwigizaji wa filamu Bongo Aunt Ezekiel amesema kuwa hafurahishwi na maneno maneno kutoka kwa wasanii hasa pale linapotokea jambo ambalo linahitaji msanii kusaidiwa au kuzikwa kwani mambo hayo yanakatisha tamaa watu wanaojitoa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hizo.

Aunty ezekile

Aunty akifurahia jambo

Steven Mengele

Steve Nyerere mwaenyikiti wa Bongo

Aunty Ezekiel

Aunty akiwa katika pozi lake

“Mambo ya ajabu sana unakuta msanii hata hajulikani na hana msaada wowote Bongo movie lakini ndio kimbelembele kulaumu watu waliojitoa mfano huyo Rammy alitoa kiasi gani? alisema Aunt Ezekiel.

Msanii huyo aliongea hayo baada ya lile sakati lilomkumba mwenyekiti wa Bongo movie ikisemekana kuwa alishindwa kuwakilisha michango ya rambirambi kwa mtoto wa Masogange na Rammy Galis kuibuka akisema kuwa atauza filamu zake kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo ndipo Aunt alipouliza ametoa kiasi gani?

Kufuatia msiba wa video Queen Agness Gelard ‘Masogange’ kusimamiwa na wasanii wa Bongo movie na kuibuka minong’ono kama kiongozi wa wasanii Steve Nyerere kulaumiwa kama hakuwakilisha rambirambi kwa mtoto wa marehemu michango ambayo ilitoka kwa wadau.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook