Your are here: Home // Habari // SIRI NYUMA YA MAUZO KIDUCHU YA FILAMU BONGO NI HUU Sehemu ya 1

SIRI NYUMA YA MAUZO KIDUCHU YA FILAMU BONGO NI HUU Sehemu ya 1

Kifo cha  filamu

Filamu ya Kibongo Komedi

TASNIA ya filamu Bongo imetengeneza nyota wengi na kukubalika lakini kwa hivi sasa hali si shwari katika soko la filamu Bongo baada ya kushudia matukio mbalimbali ya wasanii wakishindwa kumdu majanga yanapowakuta, inawezekana katika kundi hili changamoto ni nyingi.

Babu Perfect

Komedi ya Babu The Perfect

Chungu cha Tatu film

Filamu ya Chungu cha Tatu ya JB

Chanuo

Filamu ya Chanuo ya msanii Madebe Lidai

Salim Ahmed

Gabo Zigamba mwigizaji wa filamu Bongo

Kituo cha Kifo film

Filamu mpya ya Kituo cha Kifo

Unaweza usizione kwa sababu ya uwakilishi wake hauwafikii wenye kupaza sauti tofauti na wale wasanii nyota kabisa ama nguli katika tasnia hiyo, King majuto alipoumwa sauti ilifika mbali hadi mijadala iliibuka na kuwa sehemu ya kukumbukwa kwao, lakini Majuto ni sehemu ndogo tu.

Haya yote yanatokana na mfumo uliopo haukuandaliwa kibiashara ilikuwa ni kama filamu ni chombo cha kuburudisha tu na baada ya hapo hakuna tena mwendelezo katika kulijenga soko la uhakika na endelevu linalokua kiubunifu na weledi zaidi huku tukifukuzana na teknolojia.

Sinema ni nini
Sinema inajengwa na vitu vitatu ambavyo ni Sinema yenyewe watazamaji (Audience) na wachambuzi (Critics) hapo tunasema tuna filamu hivyo suala la Ubunifu (Creativity) ndio mwanzo wa utengenezaji wa fedha nyingi katika tasnia ubunifu unaolindwa ujenga thamani katika tasnia.

Soko
Kwa hivi sasa kuna changamoto inasemekana kuwa soko limetekwa na Wauzaji wa filamu kutoka nje ambazo ndio zimetawala soko letu, mbaya zaidi kile ambacho ndio ilikuwa alama ya mauzo kwa maana ya Lugha ya Kiswahili ndio inatumika.

Wauzaji wa filamu za ndani wanalalamika kuwa kama isingekuwa kutafsiri sinema za nje ambazo hata hazilipiwi kodi kwa mamlaka ya mapato Tanzania, hazikaguliwa na Bodi ya Filamu wala kupewa hakimiliki na hakishiriki na Cosota, soko lisingeyumba.

Pamoja na hayo lakini wadau wa tasnia ya filamu wanaenda mbali zaidi kwa kuuliza je soko linaweza kusimama katika changamoto kama hadithi mbovu, ulipuaji wa kazi, makosa ya kiuandishi?

Soko letu tayari wazi limeshindwa kufukuzana na Teknolojia siri kubwa ya mauzo ya filamu Duniani hakuna mauzo tena ya Dvd, kwani kuuza katika mfumo huo, una changamoto kubwa kupambana na wezi wa kazi za filamu, kwa kuendelea kutumia njia mbovu ya uzalishaji wa Dvd kumesaidia mdororo wa soko hilo.

Ili uweze kuuza lazima utumie mifumo inayotumika na tasnia kubwa na zilizofanikiwa kama Hollywood, Bollywood na Nollywood ambao wao wamefanikiwa katika kuzalisha filamu nyingi Ulimwenguni na kushika soko baadhi ya maeneo, wanaingia hapa kwa sababu nao ni tasnia ambayo inavuma duniani.

Hatua ya kwanza kabisa ili uuze kwa faida ni lazima kuwa na mastudio makubwa ya uzalishaji wa filamu yanayoshikiliwa au kumilikiwa na makampuni makubwa ya usambazaji, kwa mfano Hollywood ambao ndio kinara wa mauzo makubwa ya filamu wana makampuni sita tu.

Makampuni haya ambayo ni 20th Century Fox, Warner Bros., Paramount Pictures, Columbia Pictures, Universal Pictures na Walt Disney Pictures ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa makapuni haya pia yamejenga utamaduni wa kugawana jinsi ya kuuza filamu kulingana na maudhui.

Makampuni haya yanauza kwa njia moja zinazofanana soko lao kubwa ni Majumba ya Sinema (Theatre), Cable Tv, Box Office, majarida machapisho kuhusu sinema, matangazo ya biashara, runinga na mazao mengine ni pamoja na uuzaji wa Vikaragosi na michezo hususani kwa kutumia hadithi husika kwa filamu na tamthilia.

Sinema ikimalizika kutengenezwa inatumia muda mwingi katika kutangazwa hivyo kampuni ya usambazaji lazima iwe na ubia na vyombo vya habari ambvyo aidha wao ni wamiliki au ufanywa kwa malipo kila kitu kinatakiwa kugeuzwa pesa hapa kwetu hatuna utaratibu huo.

Na kama kuna kumbukumbu wakati filamu ikianza Bongo watayarishaji walianza vinzuri kwa kuwekeza katika matangazo, ikianiza katika magazeti , Televisheni na Redio hilo lilifanyika katika filamu ya Girl friend na baadae filamu ya Johari iliyowatoa Ray, Kanumba na Johari kutoka katika Maigizo ya Tv.

Jambo hilo halikwenda mbali zaidi baada ya kuona kuwa filamu ambazo zilikuwa zinashikiria soko letu za Kinaijeria, India na za kizungu, lakini pia katika kuijengea thamani tasnia (Branding) watayarishaji walijengea wasanii majina badala ya tasnia hilo ndilo limezalisha kufa kwa tasnia.

Kuna baadhi ya watu wasiotaka kufanya utafiti kwa kina huwa wanaamini kuwa kifo cha mwigizaji mahiri Steven Kanumba ndio kushuka kwa tasnia ya filamu, kumbe watayarishaji walifanya (Branding) kwa wasanii badala ya kuijengea thamani ya tasnia.

Nikiri wazi kuwa ubunifu aliokuwa nao marehemu Kanumba wasanii wetu hawana kabisa, ukiangalia sinema kama This is It na Big Daddy zilionyesha uwezo mkubwa kama msanii katika kuliangalia soko hatuna tena filamu za watoto zilizotengenezwa au kulingana na matukio.

Wasanii wetu wamebaki na sehemu moja tu kutengeneza idadi kubwa ya mashabiki katika mitandao ya kijamii japo sina hakika kama inawalipa kulingana na matumizi yao, harakati za jinsi gani soko la filamu kukaa sawa hawana habari nayo kwao njia pekee ni kulalamika tu.

Mwalimu wangu aliwahi kunieleza kuwa lazima kujifunza maarifa na ukishindwa kubuni cha kwako iga kwa ufasaha na watu waamini kuwa ni chako bila kukosea, wasanii hawana habari kuhusu mabadiliko ya tasnia ya filamu Duniani, hatuna kampuni iliyoweka mapato yake hadharani ya mauzo ya filamu Bongo.

Mfano kampuni kubwa kama Warner Bros. Pictures iliingiza $5.03 billioni kwa kuingiza filamu The Hobbit: The Desolation of Smaug, Gravity, na Man of Steel. Hizi ni filamu kulingana na mahitaji ya soko kampuni hiyo ndio wasambazaji wa tamthilia ya Harry Potter, The Superman, The Matrix series na Star Wars.

Kwa mfano huu unaona jinsi gani sisi tunavyokwama kwa kung’ang’ania aina moja tu ya mauzo huku ambayo ni Dvd na kwenye Runinga kwa kusubiri kwanza hadi Dvd ifeli na tayari limeshatokea, kwani kampuni kama Steps Entertaiment Ltd, hajaweza kufikia mfumo huo unaofanya vizuri duniani.

Hapo nilikuwa najaribu kuonyesha uwezo wa kampuni moja tu kati ya kampuni sita kubwa ambazo wenyewe wanaziita The Big Six Distributors, hivyo tunahitaji makampuni ambayo yanaweza kuwa na uwekezaji mkubwa kwani tasnia ukiiangalia kwa jicho la kibiashara inalipa zaidi.

Usikose Muendelezo wa Makala hii by FC

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook