Your are here: Home // Habari // CHAMA CHA WAIGIZAJI KINONDONI (TDFAA) NI ZAIDI TAFF!

CHAMA CHA WAIGIZAJI KINONDONI (TDFAA) NI ZAIDI TAFF!

Jaffary Makatu, William Mtitu

kATIBU MTENDAJI MAKATU TDFAA akimkabidhi fomu ya uanachama W. Mtitu mkurugenzi wa 5 Effect

KWANZA naanza kwa pongezi kwa uongozi wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (TDFAA) uongozi huo ambao upo chini ya Ally Baucha umejijengea thamani kubwa kwa utendaji wake katika kusaidia wasanii, kazi nzuri inayofanywa na katibu Mtendaji Jaffary Makatu akishirikiana na Masoud Kaftany hongera.

Makatu Jafary , Masoud Kaftany

Uongozi wa TDFAA ukiwa umemtembelea mwanadada Wakonta Mbezi na kumpatia kadi ya Bima ya Afya

Jaffary Makatu

Katibu bora kabisa Bongo Movie Makatu kazini.

jaffary Makatu, kulwa Kikumba

Makatu katibu mtendaji TDFAA akimkabidhi fomu ya uanachama Mwigizaji Dude ofisini kwao.

Wakonta Kapunda, Masoud Kaftany, Jaffary Makatu

Afisa HabariWakonta na Katibu katika picha ya pamoja nyumbani kwa Wakonta Mbezi Kimara

Katibu Makatu amekuwa ni mhimili muhimu sana kwa tasnia ya filamu Tanzania mara kadhaa tumeshuhudia akiwa mbele katika kuhakikisha anasaidia wasanii katika kulinda maslahi yao lakini pia kuwaelimisha katika utendaji wa kazi zao za kiuigizaji, pia ndio mhamasishaji kujiunga na chama.

Vyama vingi vimelala havipo hai jambo ambalo linaonyesha kuwa vimeshindwa kuonyesha au kutafsiri majukumu yao ambayo yamewaweka katika nafasi hizo, ni tofauti kabisa na TDFAA Kinondoni watu wawili sawa na watu 2000 namuongelea Katibu akiwa karibu na msemaji wa chama hicho.

Nimeona mengi yakifanyika na watendaji hawa hasa katibu bwana Makatu akiwa pembeni na Shemeji yangu Kaftany wakijitoa kuijenga tasnia, wakifanya makubwa kama kuwakatia Bima za Afya wasanii japo kwa mbinde lakini hawajakata tamaa ni Dira ya Uongozi bora.
.

Jafary makatu, William Mtitu

Katibu Mtendaji wa TDFAA Kinondoni Bw. Makatu akimkabidhi Mtitu fomu ya uanachama

Pia sifa ya uongozi wa Kinondoni umeonyesha kuwa na ushawishi mkubwa ni pamoja na kupewa jukumu la wao kuunda kamati kwa kushirikiana na Shirikisho la Filamu Tanzania, kamati hiyo inafuatilia mikataba ya wasanii, sherehe, maafa na maadili ikiwa agizo la Dkt. Mwakyembe waziri mwenye dhamana.

Moja ya nguvu ya utendaji ni pale ambapo hata wasanii walio nje ya mkoa wa Kinondoni wakijiunga nacho na mfano unaweza kuona msanii mkongwe kama Natasha anaishi Temeke lakini nilishuhudia akichukua kadi ya uanachama hapa, ni kazi kwa Shirikisho kuwaamsha vyama vingine view na utendaji kama hawa.

Wengine wanasema kuwa kwa sasa Chama cha Waigizaji Kinondoni inaweza kuwa ni zaidi ya TAFF chombo cha juu ambacho kina uwezo wa kuwajenga wasanii lakini hakikpo hivyo kwani imekuwa ni sehemu ya vita mipango isiyomalizika migogoro inayozimwa kwa ajili ya kupitisha jambo Fulani.

Uongozi usio na kipato ni mtihani hili ndio linalotufanya kuwapongeza sana TDFAA Kinondoni kwa juhudi zao bila kuchoka pamoja kufanya kazi bila kipato ni kipaji na upendo wa hali ya juu kuwa na viongozi wenye hali na moyo mkubwa, tukishauri pia vyama vingine vifuate nyayo.

Kwani idadi kubwa ya wasanii nyota wamejiunga na chama hiki ikiwa vyama vingine ni wakati wa kujitathimini kwa ajili ya kusaidie tasnia ikue tofauti na hali ilivyo kwa sasa.

Niliona jinsi Kinondoni ilivyopigania suala la Mzee King Majuto hadi kuondoka ni alama kubwa sana kwa wanatasnia pengine ningetarajia chama cha Waigizaji Mkoa wa Tanga kulifanikisha jambo hilo, lakini niliona jinsi Makatu na Kaftany walivyopigana hiyo ndio tasnia tuitakayo.

Imeandikwa na FC

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook