Your are here: Home // Habari // BONGO PAMEBANA SANA BORA KENYA–DUMBA

BONGO PAMEBANA SANA BORA KENYA–DUMBA

Issa Mndeme

Dumba mwigizaji wa filamu Swahilihood.

MWIGIZAJI wa filamu Bongo Issa Mndeme ‘Dumba’ anasema kuwa sanaa kwa sasa haiangalii ubora wa kazi baada ya hali ya kazi za filamu kuwa ngumu hivyo mtayarishaji inatakiwa aangalie soko nje ya mipaka ya Tanzania ukilenga kuuza hapa utafeli tu.

Issa Mnndeme, Tina Mroni

Wasanii wa Tamthilia Upande wa Pili

Issa mndeme

Dumba akiwa katika pozi la picha

Issa mndeme , tina mroni

Wasanii wa tamthilia ya Upande wa Pili wakiwa katika picha ya pamoja.

“Sanaa tunaipenda lakini, tumefanikiwa kurekodi tamthilia yetu ya Upande wa pili itaonyeshwa nchini Kenya kupitia Citizen Televisheni baada ya hapa kushindwa kuelewana na televiesheni,”alisema Dumba.

Mndeme ni msanii wa filamu na mwanamuziki wa asili anaomba wawekezaji kuingia pia kuwekeza katika filamu kama wanavyowekeza katika muziki wa kizazi kipya ili kuwe na uwiano unaolingana kwani ajira zitaongezekana na kuondoa ugumu suala la ajira Bongo.

Watengenezaji wa tamthilia Bongo kwa sasa inawalipa wanapofanikiwa kuingia mikataba na Runinga za nje na si za ndani kwani malipo yake ni kiduchu sana kuliko zile za nje ni changamoto kwa taasisi husika kushindwa kutengeneza mazingira kwa wadau wake .

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook