Your are here: Home // Habari // WASANII BONGO MOVIE WANAHITAJI USIMAMIZI -LAMATA

WASANII BONGO MOVIE WANAHITAJI USIMAMIZI -LAMATA

Leah Mwendamseke

Lamata muongozaji wa filamu Swahilihood.

MUONGOZAJI mahiri wa filamu Bongo Leah Mwendamseke ‘Lamata’ anaamini kuwa hakuna msanii wa filamu anayeweza kusimama katika tasnia bila kuwa na usimamizi kutoka kwa menejimenti inayojishughulisha na masuala ya filamu tena yenye ndoto za kimataifa.

Leah Mwendamseke

Lamata akiwa katika pozi la picha.

Leah Mwendamseke

Lamata muongozaji na mtunzi wa filamu Swahilihood.

Lamata ndio mungozaji mwenye ushawishi na kiuongo kikubwa kwa wasanii nyota Bongo Movie kwani ana uwezo wa kuwaunganisha wasanii wenye majina katika filamu moja pia ndio mzalishaji wa nyota kama Hemed, Mutrah, Tausi Mdegela na nyota kibao.

“Kwetu changamoto ni nyingi sana kama mimi nina wasanii wengi ambao wananitegemea niwape kazi hivyo moja ya jukumu langu kuhakikisha wote wanaigiza lakini kuwasimamia ndio tatizo,”alisema Lamata.

Lamata amejizolea umaarufu kwa utunzi na uongozaji wa filamu hasa za wasanii nyota huku akiwasimamia wasanii kama Jack Wolper, Kajala Masanja, Taiya Odero mwanadada huyu anajivunia kutengeneza tamthilia ya Kapuni inayoruka Dstv kwa kushirikisha wasanii wengi wenye majina makubwa.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook