Your are here: Home // Habari // SARAH ALIA NA BODI YA FILAMU KWA UPENDELEO!

SARAH ALIA NA BODI YA FILAMU KWA UPENDELEO!

Sarah Nyika

Sarah Nyika mwigizaji wa filamu Swahilihood.

MWIGIZAJI wa filamu wa kike Sarah Nyika afungukia kufungiwa filamu yake ijulikanayo kwa jina la Imebuma kuwa ni upendeleo unaofanywa na Bodi ya Ukaguzi wa filamu kwa watayarishaji Chipukizi na badala yake kupendelea filamu za wasanii au watayarishaji wenye majina makubwa.

Sarah Nyika

Sarah akiwa katika pozi

Sarah nyika

Sarah Nyika

Sarah Nyika

Sarah Nyika mwigizaji wa filamu Swahilihood.

Msanii huyo amedai kuwa pamoja na marekebisho aliyoambiwa afanye na Bodi alifanya lakini aliporudi tena akapewa barua ambayo imeifungia sinema yake na akaambiwa kuwa kama hajaridhika na majibu akate rufaa kupata kibali cha ukaguzi

“Sasa ni mwaka wa pili toka kuhangaikia filamu yangu ya Imebuma kuzuiwa na Bodi ya Filamu eti, haina maadili lakini filamu zile ambazo wameigiza ushoga zimepitishwa,”alisema Sarah.

Mtayarishaji huyo amezidi kuelezea kuwa filamu yake hiyo imeelezea tabia ya kijana mmoja ambaye ana tabia za kike anapenda kushinda na wanawake lakini si shoga pamoja na kutoa vipande ambavyo aliambiwa mwisho kanyimwa kibali wakati filamu ya Shoga yangu ya Tino imeonyesha ushoga na imepita.

Sarah analalamikia ukwamishaji huo umemwingiza gharama kubwa ambayo hana kitu cha kulipa kwani fedha hizo alizikopa banki na kuingiza katika filamu zimepotea na hajui atazirudishaje wakati sinema hajauza ipo ndani tu, ikisubiriwa maamuzi.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook