Your are here: Home // Habari // SIDE WA KITONGA ASHIKWA PABAYA KITAANI

SIDE WA KITONGA ASHIKWA PABAYA KITAANI

Said Mbelemba

Side mchekeshaji wa Sise wa Kitonga

MCHEKESHAJI Nyota katika kipindi cha Side wa Kitonga Said Mbelemba ‘Side wa Kitonga’ anasema kuna wakati anapata wakati mgumu anapokutana na baadhi ya wapenzi wa kazi zao kupitia Televisheni hasa pale ambapo uamini kuwa matukio yaonyeshwayo ni halisi.

Said Bakary Mbelemba

Side akiwa katika pozi la picha

Said Bakary Mbelemba

Side akifanya mahojiano na E Fm Radio akiongelea show ya Side wa Kitonga

“Najitahidi kuzoea hali kuna wakati nakuwa na wakati mgumu sana hasa pale ninaokuwa nimeigiza tukio ambalo linaonekana kama la unyanyasaji kwa wanawake, unaweza kusikia mhuni sana Yule,”alisema Side.

Msanii huyu ambaye ni mtoto wa mwigizaji na mchekeshaji mkongwe Bongo Mzee Jangala anasema kuwa uhusika wake katika Side wa Kitonga ni kijana anayependa kulelewa na wanawake wenye fedha zao, hivyo mara nyingi huwa ni mtu wa mikasa kufumaniwa, kunusurika kupigwa akiigiza kama mhusika mkuu.

Side wa Kitonga uruka kupitia Runinga ya E Tv kila siku ya jumatano saa 3:30 usiku, show hiyo inapambwa na kupendeza zaidi Side akiwa na swahiba yake Kalombo ndani ya saluni uendesha kazi yao kwa kuburudisha na kuelimisha mashabiki wao mwanzo wa show hadi mwisho.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook