Your are here: Home // Habari // NAFURAHIA KAZI ZA MIKONO YANGU – SHILOLE

NAFURAHIA KAZI ZA MIKONO YANGU – SHILOLE

Zuwena mohamed

Shilole Mwigizaji wa filamu na mwanamuziki

ZUWENA Mohamed ‘Shilole’ anasema anafurahia kutengeneza fedha kwa mikono yake mwenyewe na hapendi kukata tamaa kwa kile chochote ambacho ukianzisha kwa ajili ya kujiongezea kipato hivyo si rahisi sana kudumaaa katika aina moja ya biashara na kujikuta akifanya kazi kulingana na mahitaji.

Zuwena Mohamed

Shilole akiwa katika vazi la kazi

Zuwena Mohamed

Shilole katika pozi

Zuwena Mohamed

Shilole mwigizaji wa filamu Swahilihood.

“Nafurahia sana kazi za mikono yangu kwani siwezi kuwa tegemezi kwa biashara moja kukwama ni rahisi, lakini sichukii hata ukiniambia mama Ntilie muhimu kupata pesa tu,”alisema Shilole.

Shilole ambaye amekuwa mahiri sana katika ubunifu anasema kuwa anamshukru Mungu kwa kumfungulia kuwa muuza chakula Shishi Food kwani anaweza kufanya kazi kulingana na nyakati, kama hivi sasa anaendana na mabailiko ya ulaji naye anapika futari kwa kukodishwa na wateja wake.

Pamoja na kufanya sanaa kwa umahiri mkubwa katika filamu na muziki lakini mwanadada huyu pia amekuwa ni mbunifu kwa upande wa chakula, kwa mfano kuzindua Shishi chili source huku akiwa mpishi mkuu katika mgahawa wake wa kisasa Kinondoni.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook