Your are here: Home // Habari // SIKU HIZI NI KAZI SI SURA TENA WAKONGWE FANYENI KAZI- DUMA

SIKU HIZI NI KAZI SI SURA TENA WAKONGWE FANYENI KAZI- DUMA

Daud Michael

Duma mwigizaji wa filamu Swahilihood

SIKU za nyuma tulizoea kusikia wasanii wa Taarab wakirushiana vijembe lakini siku hizi hata huku kwetu katika tasnia ya filamu mambo yameiva, mwigizaji Daud Michael ‘Duma’ anasema kuwa soko la sasa la filamu halihitaji umaarufu au ukongwe zaidi ya uigizaji bora.

Daud Michael

Duma mwigizaji wa filamu Swahilihood.

Daud Michael

Duma msanii wa filamu Swahilihood.

“Siku hizi watu wameamka wanataka kazi bora si sura ya msanii gani ambaye yupo katika tasnia toka zamani unatakiwa kuigiza kisasa na ufanye kazi si porojo kama zamani majina yaliwalinda,”alisema Duma.

Duma anasema kufuatia kizazi kipya kuishika tasnia ya filamu baadhi ya wasanii wa zamani wamebaki na majina ambayo kuna wakati wanashindwa kuyalinda wanabaki wakilalamika badala ya kubadilika na kukimbizana na sanaa inayokwenda na wakati mabadiliko muhimu.

Siku za nyuma tumeshuhudia msanii huyu akijaribu kumshutumu msanii mwezake wa filamu Gabo akidai kuwa hajui kuvaa kama msanii maarufu tukio ambalo lilizua mjadala, na kuzalisha makundi mawili yakirumbana kwa kuhusu wasanii hao wawili wakidai kuwa waonyeshe kazi na si maneno.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook