Your are here: Home // Habari // DR. ALMASI ANAIMBA HIP HOP HAJALI UMRI WAKE!

DR. ALMASI ANAIMBA HIP HOP HAJALI UMRI WAKE!

Steven Almasi

Dr. Almasi mwigizaji wa filamu Swahilihood

MWIGIZAJI wa filamu Bongo Steven Almasi maarufu kama Dr. Almasi anatamba kuwa pamoja na kuwa ni msanii mwenye umri mkubwa ameamua kuonyesha kipaji chake kingine cha uimbaji kwa kuimba muziki wa kizazi kipya na kufanikiwa kurekodi nyimbo kadhaa hadi sasa na kuwaduwaza mashabiki.

Steven Almasi

Dr. Almasi katika pozi

Steven Almasi

Dr. Almasi mwigizaji wa filamu Bongo

Steven Almasi

Dr. Almasi akiwa yupo tayari kwa kazi yake ya sanaa.

“Ukisikia Dr. Almasi anaimba matarajio yako utajua labda anaimba muziki wa Kwaya no, nafanya Hip Hop wengi hawaamini lakini wakipata bahati ya kusikiliza kila msanii anataka nifanye nao kazi lakini No,”alisema Dr. Almasi.

Dr. Almasi amedai kuwa pamoja na changamoto inayojitokeza hawezi kuachana na muziki wa hip hop kwani upo katika damu yake amechelewa tu kurekodi na kama itatokea mtu kumshangaa na kumcheka itakuwa ni sawa na promotion kwake kwani kajiandaa kwa hilo na atafanya maajabu,

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook