Your are here: Home // Habari // BODI YA FILAMU YAMPONGEZA JOKETI MWEGELO

BODI YA FILAMU YAMPONGEZA JOKETI MWEGELO

Joketi Mwegelo

Mh. Joketi Mwegelo mwigizaji wa filamu Swahilihood

KATIBU wa Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Bi. Joyce Fissoo amewapongeza waigizaji wa kike kwa mwaka huu kuwa ni wasanii wa mafanikio kwa kufanya vizuri katika kazi zao na kupata nafasi mbalimbali katika uongozi na kushinda tuzo za filamu sehemu tofauti tofauti.

Joyce Fissoo

Bi. Fissoo katibu mtendaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania.

Joketi Mwegelo

Joketi Mwegelo mwigizaji

Joketi Mwegelo

Joketi Mwegelo mwigizaji mkuu wa Wilaya mteule

“Mwaka huu umekuwa wa bahati kwa waigizaji wa Tanzania husasani wa kike Monalisa alishinda tuzo nchini Ghana lakini pia kualikwa Marekani katika tuzo Joketi amekuwa kiongozi sina budi kuwapongeza,”alisema Bi. Fissoo.

Bi. Fissoo amempongeza Joketi Mwegelo kama msanii mwigizaji ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe msanii huyo alishiriki katika filamu ya Mikono Salama ya Jb na Filamu ya Chumo ya MFDI akiwa na marehemu Sharomilionia pia aliratibu ujio wa msanii wa Naijeria Noah Ramsey.

Mama Fissoo kama mtendaji mkuu kwenye tasnia ya filamu amesema kuwa kuchaguliwa Joketi na Mh. Dkt. John P. Magufuli kuwa mkuu wa Wilaya ni hatua nzuri kwa tasnia na kuaminiwa kwa wasanii nchini, hivyo kwa niaba ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza anampongeza msanii huyo.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook