Your are here: Home // Habari // NILICHOMWA NA CHUPA KINYAMA NI MUNGU TU– MASINDE

NILICHOMWA NA CHUPA KINYAMA NI MUNGU TU– MASINDE

RICHARD MSHANGA

MASINDE MWIGIZAJI WA FILAMU SWAHILIHOOD.

MWIGIZAJI wa filamu na tamthilia mkongwe nchini Tanzania Richard Mshanga ‘Masinde’ amefunguka kwa kusema kuwa tukio la yeye kushambuliwa na kujeruhiwa ni kitu cha ajabu na hadi leo hajapata jibu mlengwa alikusudia nini kumshambulia na kumchoma na chupa shingoni na katika kidevu.

Richard Masinde

Masinde mwigizaji wa filamu Swahilihood

Richard Masinde

Masinde katika pozi la picha

“Mara nyingi tumezoea kuona vibaka wakivamia watu kuwajeruhi kisha kuwapora mali zao lakini si kwa huyu aliyenivamia na kutaka kuniua kwa kutumia chupa ni ukatili wa aina yake,”alisema Masinde.

Masinde anasema kuwa anashukru kwani mtuhumiwa amekamatwa na muda wowote atapandishwa kizimbani kujibu tuhuma kufanya shambulio la kudhulu, Masinde alikutwa na majanga hayo eneo la Manzese na kupatiwa matibabu Zahanati ya Tandale na kuhamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala ameruhusiwa yupo kwake Kitunda.

Suala la msanii huyo lipo mahakamani na mtuhumiwa amekamatwa yupo lupango ikisubiriwa siku atakapoitwa kusikiliza kesi yake, pia Masinde ameomba msaaada wa kisheria kusimamia kesi yake kwani haamini kuwa kapona na hajajua mlengwa alikusudia kitu gani kumjeruhi bila kuchukua kitu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook