Your are here: Home // Habari // WADAU WA SEKTA YA FILAMU MKOANI SONGWE ANDAENI FILAMU ZA KIUTAMADUNI

WADAU WA SEKTA YA FILAMU MKOANI SONGWE ANDAENI FILAMU ZA KIUTAMADUNI

Wadau wa filamu Vwawa Songwe

Wadau wa filamu wa Vwawa katika semina Mkoani Songwe

Na Anitha Jonas – Vwawa,Mbozi
Songwe
Wadau wa sekta ya Filamu Mkoa wa Songwe waelezwa kutumia fursa zilizoko Mkoani hapo ikiwemo uwepo wa maeneo mazuri ya asili naya kiutamaduni kwa ajili ya kuandaa filamu za Kiutamaduni.

Joyce Fissoo, Nicholaus William, Juma Mhina

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William (katikati) akiwataka wadau wa sekta ya Filamu Mkoani Songwe (hawapo pichani) kutumia fursa za kiutalii na mazingira mazuri ya Mkoa huo kuandaa kazi za filamu alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau hao iliyofanyika Mjini Vwawa Wilayani Mbozi,kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bw.Juma Mhina.

Joyce Fissoo

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akionyesha moja ya leseni inayotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania kwa wadau wa sekta ya filamu Mkoa wa Songwe (hawapo pichani) zinazotolewa na Ofisi yake kwa waandaaji wa kazi za filamu nchini katika madaraja mbalimbali kulingana na uzoefu, katika warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau hao iliyofanyika leo Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi Mkoani hapo .

Dr. Vicensia Shule

Mmoja wa watoa Mada Dkt.Vicenisia Shule akitoa Mada ya Uandaaji wa Miswada ya Filamu kwa wadau wa sekta ya filamu Mkoani Songwe (hawapo pichani) katika warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Bodi ya filamu Tanzania iliyofanyika Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi kwa lengo la kuwajengea uwezo wasanii hao.

Joyce Fissoo

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo (kulia) akisikiliza swali la mmoja wa wadau wa sekta ya filamu mkoani Songwe Bw.Barick Mbogella aliyehudhuria warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya felamu mkoani hapo, iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika leo katika Mji wa Vwawa,Wilayani Mbozi.

Tegemea Hasunda, Joyce Fisssoo

Katibu Umoja wa Wanatasnia wa Filamu Mkoa wa Songwe Bw.Tegemea Hasunga akichangia mada ya uandaaji wa Miswada ya kazi za filamu katika warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu Mkoani Songwe iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika leo Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi.

Bicco Mathew, Juma Mhina,

Baadhi ya wadau wa sekta ya Filamu Mkoa wa Songwe wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William aliyeketi meza kuu (wapili kutoka kulia) mara baada ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu wa mkoa huo,yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi,A kutoka kushoto wa pili Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na kutoka kulia wapili ni Kaimu Afisa Tawala Mkoa wa Songwe Bw. Juma Mhina na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw.Mathew Bicco.

Bicco Mathew, Juma Mhina

Baadhi ya wadau wa sekta ya Filamu Mkoa wa Songwe wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William aliyeketi meza kuu (wapili kutoka kulia) mara baada ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu wa mkoa huo,yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi,A kutoka kushoto wa pili Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na kutoka kulia wapili ni Kaimu Afisa Tawala Mkoa wa Songwe Bw. Juma Mhina na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw.Mathew Bicco.

Kauli hiyo imetolewa leo Wilayani Mbozi, Mjini Vwawa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoanI Songwe.

“Mkoa wa Songwe umebarikiwa kwa kuwa na fursa nyingi ikiwemo uwepo wa Kimondo ambacho ni kivutio kikubwa cha utalii pamoja na mandhari nzuri ya mkoa huu ambayo imekuwa ni kivutio kikubwa kwa wapiga picha wa kimataifa wanaokuja kupiga picha katika mkoa huu kwa ajili ya kuandaa Makala mbalimbali,”alisema Bw.William.

Akiendelea kuzungumza katika warsha hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa ni lazma kazi za filamu kuandaliwa kwa uweledi ili sekta ya filamu nchini iweze kushindana vyema na soko la filamu Afrika na Duniani kwa ujumla na kwa kuzingatia hilo filamu zenu zitaweza pia kushinda tuzo za kimataifa.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo alitoa elimu kwa wadau hao wa filamu kwa kuwaeleza majukumu ya bodi ya filamu pamoja na kuwaeleza kuwa bodi ya filamu imekuwa ikitoa leseni na vitambulisho kwa ajili ya utambulisho wa wadau wanaojihusiha na kazi za filamu na hifadhi kanzi data ya wadau wa filamu nchini.

“Suala la ukaguzi wa kazi za filamu kwa mikoani kuanzia ngazi ya miswada inakaguliwa katika Halmashauri kupitia bodi zilizoundwa kupitia Afisa Utamaduni pamoja na wajumbe mbalimbali hivyo msanii wa mkoani mswada wa kazi yake ya filamu na filamu yake inakaguliwa nao na halazimiki kuja mpaka Dar es Salaam,”alisema Bibi Fissoo.

Pamoja na hayo Katibu Mtendaji huyo alieleza kuwa warsha hiyo itatoa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo somo la Uandaaji wa Miswada ya Filamu,Somo la kijitangaza (Branding),Matumizi ya Mitandao na Matumizi ya lugha ya Kiswahili na masomo mengine yanayosaidia sekta ya filamu.

Mbali na hayo nae mmoja wa wasilishaji mada ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Filamu nchini Dkt. Vicenisia Shule aliwaeleza wadau hao wa filamu kuwa serikali inandaa Sera ya Filamu ambayo itasaidia kutoa mwongozo wa kuisimamia vyema sekta ya filamu kwa kuzingatia sheria inayosimamia sekta ya filamu nchini kwa sasa.

Hata hivyo warsha hiyo ilimazika Julai,20 mwaka huu ambapo sherehe za ufungaji zilifanywa na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook