Your are here: Home // Habari // HAIJAWAHI KUSIMULIWA BURIANI KING MAJUTO!

HAIJAWAHI KUSIMULIWA BURIANI KING MAJUTO!

Amri Athuman

King Majuto mwigizaji wa filamu bongo

. Ameandika filamu 500
. Ameshiriki zaidi ya Filamu 1,500 kafariki kabla ya Ndoto yake ya kununua Trekta
. Alikuwa Mtumishi wa Serikali
Nikiwa nimejitupa kitandani usiku unaingia ujumbe katika simu yangu ukiuliza eti ni kweli King Majuto amefariki? Nachelea kujibu kwani toka kuanza kuugua kwa gwiji huyo wa Tasnia ya filamu na uchekeshaji alizushiwa mara nyingi kifo, nikatafakari na kuamua kumpigia Ahmad ambaye nilimwacha Hospitali.

Bodaboda Tanga

Msafara wa Bodaboda kuelekea Kiriku kwa King Majuto

Msiba wa King Majuto

Msafara wa waombolezaji wakimsindikiza King Majuto

Jacob Stephen

Mwigizaji JB akiwa na waombolezaji msiba wa King Majuto Tanga

King Jb 531

Amri Athuman, Dr. Harrison Mwakyembe

Dr. Harrison Mwakyembe alipomtembelea King Majuto Hospitali ya Taifa Muhimbili akijiandaa kwenda ktk matibabu India

waombolezaji Tanga

Waombolezaji nyumbani kwa King Majuto Donge Jijini Tanga

Shamsa Ford

Wasanii wa Bongo movie Shamsa Ford akiingia nyumbani kwa King Majuto

Waombolezaji

Waombolezaji Jijini Tanga

Amri Athuman

King Majuto mwigizaji wa filamu enzi za uhai wake

Mkwere, Sumaku Kabuti Onyango

Wachekeshaji Mkwere, Sumaku kutoka Mizengwe walikuwepo msibani Tanga

Martin Shegela

Naibu katibu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Nicholaus Mkpa na mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin

Waombolezaji Jijini Tanga King Majuto

Kundi la waombolezaji wakiwa na huzuni kwa kuondokewa na mwigizaji wampendao King majuto

Sikuongelea kifo lakini alipopokea tu simu akanijulisha kuhusu kifo cha Amri Athuman almaarufu kama King Majuto baada ya kudhibitisha naondoka haraka kuelekea katika tukio huku nikikumbuka mengi ambayo nilikuwa nikiongea naye tukiwa na ahadi akipona tutengeneze Makala(Documentary) ya maisha yake.
Lakini ni wakati uliwadia ilimpasa kuondoka ili sisi tujifunze kupitia kwake, kwani hadi sasa wakati yeye alikuwa tajiri wa Roho mwenye kanzi data kubwa ya mashabiki jamii na baadhi watendaji wamekuwa wakilalamika kuwa msanii huyo pamoja na kuwa na jina kubwa ni maskini jambo ambalo yeye amekuwa akilipinga kila mara.
Nami naungana na King Majuto kuamini kuwa kumbe ni zaidi ya tajiri mwenye fedha nyingi Duniani kwani yeye ni mtu mwenye mashabiki wengi pengine kuliko wale wanaoweza kupata mashabiki kwa nafasi zao kiuchumi na kidola, kwani msiba wake haukuwa na bakuli.
Kama mnavyojua mara nyingi inapotokea msiba wa msanii hutumika nguvu nyingi sana katika kuchangishana ili kuufanya kuwa msiba wa kitaifa lakini halikufanyika kwa King Majuto hivyo kuwa tukio lisiloacha watu kusutana na kunyoosheana vidole kwa kutambaa na michango ya rambirambi mitini.
Nakumbuka siku moja tukiwa Hospitali hayati King alikuwa akituchekesha sisi tuliona ni utani lakini kumbe alikuwa akimaananisha kuwa alichoongea kina mantiki na kifuatwe na kimefuatwa na waliobaki alisema hivi.
“Nikifa hakikisheni narudishwa Tanga na siku ya Ijumaa nikazikwe shambani kwangu Kiriku, sitaki kupelekwa Leaders Club kuangwa na masuti meusi ya nini?
Watu walicheka lakini ndio kilichotokea kwani siku ya jumatano baada ya umauti kumfika siku ya pili aliagwa katika viwanja vya Karimjee na safari kuanza mida ya saa kumi, ndio sasa ile kauli yake ya kusema yeye ni tajiri wa jamii ilipoonekana kwani kila kijiji raia hawakujali usiku walisimama barabarani.
Hawakusimama barabarani tu bali walikuwa wanazuia magari na kuomba msafara usimame na wafanye Dua mpakani mwa Pwani na Tanga kijiji cha Manga walikuwa wa kwanza awali ilikuwa mshangao kwetu tuliokuwa katika msafara lakini baada ya hapo kila kijiji utaratibu ulifuatwa.
Sehemu zilizoshiriki kutoa huduma hiyo ni Mkata, Komkonga, kwedikwazu, Kabuku, Kwachonga, Kwedizinga, Ugweno, Michungwani, Hale, Maguzoni, Kwabastola, Mpakani, Muheza, Lusanga, Kitisa, Tanganyika, Mkanyageni, Kilapula na Pongwe.
Maeneo mengine ni Bagamoyo, Saruji, Kange, Majani mapana, Mwamboni, Kwamichi, Mabanda ya Papa, Pangani Road, Makororo sokoni hatimaye kuingia mtaani kwake Donge akipokelwa kwa huzuni kwa mara nyingi ule useme wa Nabii hakubaliki kwao kwa King unafutika.
Tujikumbushe Mahojiano yake awali kabla kifo chake kwani aliongea mengi sana, King Majuto ameondoka akiwa bado ndoto yake ya kununua Trekta kwa ajili ya kilimo cha kisasa haijakamilika fuatilia Interview hii:-

Je una sinema ngapi?
King Majuto: Nina sinema zaidi ya mia tano nilizoandika kwa mkono wangu nilizoshiriki zaidi ya 1,500 hadi majina nimesahau.
Je Ulianza lini kuigiza?
King Majuto: Nilianza kuigiza mwaka 1958 nikiwa na miaka kumi tu lakini kujulikana na kuwa maarufu ilikuwa ni mwaka 1983 nilipoitwa na kuajiriwa na kundi la Dar es salaam Development Corporative (DDC Kibisa)
Kwanini unajiita King Majuto?
King Majuto Jina la King Majuto nikiwa DDC Kibisa ndio lilipozaliwa jina hili nililipata kutokana na umahiri wangu wa kuigiza filamu za kuhuzunisha wakawa wananiita King Majuto wenzangu wa DDC Kibisa.
Je uliwahi kumiliki kundi lako la maigizo?
King Majuto: Sijawahi na sikupenda kuwa na kundi kutokana ugumu wa kuendesha kundi, tofauti ya filamu na vikundi ni moja ukiwa na kundi unategemewa na wasanii kuhusu mahitaji yao yote, ikiwa Malazi usafiri nk. lakini filamu unaweza kuwaambia tucheze tukiuza tutagawana, kikundi itabidi ujue kwa kutoa pesa na kuwalipa kama ni mshahara wao au posho.
King wewe ni zao bora lililotokana na uwepo wa Makundi ya michezo ya Jukwani kwa sasa hayapo tena je kwa mwenendo huu nini hatima ya sanaa ya uigizaji Tanzania?
King Majuto: Huu mwenendo tunaoenda nao wa kutupa au kupuuzi sanaa za Maonyesho ni mbaya, kwa sababu watu hawawezi kuona umuhimu vitu vya Mila na tamaduni zao zaidi ya kuona yooyoo wewe wangu mimi nakupenda sana ,,, hawawezi kuona umuhimu wa ngoma au maigizo ya kwetu zaidi ya vitu vya Magharibi. Tulitarajia kuona ngoma ya Kingoni, Kimakonde na nyinginezo hamna tena .

Amri Athuman

Hayati King Majuto enzi za uhai wake

Je kwa sasa kuna sehemu au kikundi kinafanya sanaa mchanganyiko kama zamani?
King Majuto: Zipo kidogo sana labda kwa mwalimu wangu Chege wanafanya maonyesho yao Makumbusho binafsi napenda sana sanaa mchanganyiko Sarakasi, maigizo, ngoma za asili, ngonjera
King Majuto kilio chako ni kulinda Mila na kutoa nafasi kwa sanaa zetu Je Mh. Rais alipokutembelea kukuona ulitumia nafasi hiyo kuongelea tatizo hilo?
King Majuto: Hapana ujue alikuja na muda ulikuwa mchache lakini niliangalia afya yangu kwanza, lakini namuamini sana Mh. Rais Magufuli kama ujumbe huu utamfikia ataufanyia kazi, kushinda kusimamia vema sana yetu tunapoteza ajira nyingi hilo la kwanza pili utamaduni wetu unakufa,
Mfano baadhi ya makampuni ukiomba ufadhili kwa ajili ya kufanya filamu au sanaa za asili hayawezi kukupatia fedha lakini wepesi kudhamini wakata viuno barabarani kwa utamaduni wa n je ni hatari sana kwa Taifa letu.

Je kati ya watoto wako kuna moja wao ambaye anaweza kukurithi na kuchukua nafasi ya kipaji chako?

King Majuto: nina watoto kumi wa kike watatu na saba wa kiume Wanangu wote ni waigizaji kasoro kaka yao mkubwa Athuman ambaye ni mwanamuziki anapiga Gitaa, wanangu kama Mohamed na Haruna wameanza kuigiza wakiwa na umri wa miaka 6 umri mdogo kuliko mimi nilivyoanza kuigiza.

Kwa sasa kila msanii analia njaa wanasema sanaa hailipi kwako hali ipoje?

King Majuto: Kwangu mimi kuigiza ni kipaji nimesomesha watoto wangu hadi Chuo kikuu kwa sababu ya Kuigiza, nimejenga nyumba tatu ni sanaa, nina shamba nzuri kwa ajili ya kuigiza, ninapendwa sana na watu Kitaifa kwa ajili ya kuigiza anayechezea sanaa au kutuzarau sisi wasanii namuona kama mwehu lazima uipende kazi yako.

Matukio ya kipekee kwa King Majuto katika msiba wake
Pamoja na kuonekana msanii huyo ni amekula chumvi nyingi huku akiwa mahiri lakini FC ilikutana na mwalim wake wa kwanza kabisa kumfundisha uigizaji Hamza Kasongo ambaye ni mjomba wake aliyezaliwa na mama yake mwenye nguvu zake ambaye anasema

“King Majuto ndio mwanafunzi wangu pekee sikuwahi kumpata msanii mwelewa na mbunifu kama yeye hivyo pamoja kuwa nimpoteza kama mpwa wangu lakini ni pengo kubwa kwa tasnia,”alisema Mzee Kasongo.

Kitu kingine cha kipekee ni msanii wa komedi aliyemuenzi kwa staili ya aina yake ni mchekeshaji Jacob mkweche ‘Ringo’ aliyekataa kupanda gari za jumuiya na kukodi pikipiki na kusafiri nayo hadi Jijini Tanga kurudi kama sehemu maombolezo yake.

“Nimeona sina njia nyingine ya kumuenzi Baba yetu rafiki yetu lakini mimi kanitoa yeye katika tasnia ya filamu nimeguswa na kuamua kumlilia kwa kupanda pikipiki hadi msibani,”alisema Ringo.

King Majuto alizaliwa tarehe 2 February 1948 elimu yake ya msingi alipata katika shule ya msingi Msambweni, 1955 hadi 1958, mwaka 1959 alisoma Shule ya St. Antony darasa 8 ambayo ndio Tanga School kwa sasa .

Kazi alifanya katika vikosi vya ulinzi na Usalama sehemu tofauti tofauti ikiwa ni katika kikosi cha Monduli, kikosi cha Lugalo, Mgulani JKT, na Kigamboni, JKT Ruvu, Jeshi la Zimamoto, Kiwanda cha Mbolea, kabla kuingia rasmi katika fani ya uchekeshaji kwa kifupi alikuwa mtumishi wa Serikali.

Mwaka 1983 ndio alihamia Dar es salaam na kujiunga na kikundi cha DDC Kibisa akipokelewa na mwalim Chege ndio ilikuwa mwanzo wa kutengana na mjomba wake mzee Hamza Kasongo ambaye alijiunga na Jeshi la JWTZ ambaye alikuwa mshauri na mwalimu wake.

Baadae alihamia Makutano Dancing Troupe, Muungano Dancing Troupe, TOT na makundi mengine aliwahi kuwa na kundi la Wami lakini baadae aliachana na umiliki wa makundi alikuwa anabaki kama mwalimu katika makundi aliyokuwa anayasaidia na ameacha kundi Jijini Tanga King Majuto Crew.

Pia alifanya kazi na Tarzan Recording Centre Tanga, aliigiza sauti katika lafudhi kama Kidigo, Kipemba, Kisambaa wakati huu ikitumika sana michezo ya Redio, pia alifanya kazi na Tanga Filmmakers, Dtv, Channel ten, Al Riyamy Production, Steps Entertainment Ltd.

Mengine ni Mt Productions, Nisha’s Film Productions, Mzee King Majuto pia alifanya kazi na makampuni kama Airtel, Neel Salt, Asas Milk, Ivory, Azam, Abood Tv, na makampuni mengine.

Funzo kwetu wasanii kufanya kazi kwa juhudi zaidi Mzee King Majuto alikuwa Mjasiriamali, msanii na mfanyakazi
Msiba wa King Majuto ilifanya Tanga kuzizima huku watu wengi wakiwa hawaamini kama kweli amefariki, ni tukio liloacha mengi ya kujifunza kwetu wasanii na wadau wa tasnia ya filamu nchini.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook