Your are here: Home // Habari // NAPATA TABU SANA KUPATA MKE- KIWEWE

NAPATA TABU SANA KUPATA MKE- KIWEWE

Robert Augustino

Kiwewe msanii wa filamu Swahilihood

ROBERT Augustino ‘Kiwewe’ amefunguka kuwa kutokana na umaarufu wake amejikuta katika wakati mgumu kumpata mke kwani wengi wao wanaojitokeza wanakuwa wanamtaka kutokana na umaarufu wake na si kwa mahaba ya kweli hivyo inamtatiza kumpa mtu ampendae.

Robert augustino

Kiwewe msanii wa filamu Bongo

Robert Augustino

Kiwewe katika pozi

Robert Augustino , Pembe

Kiwewe na mwigizaji mkongwe Pembe aliyeshiriki katika filamu ya Vurugu mechi

Vurugu Mechi Film

Filamu ya vurugu mechi ya Kiwewe

“Nimejikuta na vipimo kwa ajili ya kutambua wababaishaji maana kuna Kiwewe na Robert sasa wanawake wengi wanamtaka sana Kiwewe sasa inavyotokea hivyo najua kuwa hapa hakuna mwanamke wa ndoa,”alisema Kiwewe.

Kiwewe anasema kuwa hiyo ndio sababu kubwa ameshindwa kuoa japo anajiona kuwa anastaili ya kuchelewa kuoa kwani hapati wanawake wanaompenda zaidi ya waigizaji lakini kama ataenda kwa pupa anaweza kuoa mke asiye na mapenzi nay eye na siku akiacha kuigiza mke naye ataondoka.

Kiwewe ambaye anatamba na The Komedi show irukayo EA Tv Channel 5 ameamua kuwasapoti wasanii wachanga na tayari ameandaa kazi moja ujulikanayo kwa jina la Vurugu mechi akiwa na kundi lake huku akishirikisha wasanii wakongwe kama Pembe Bin Kichwa, Bambo, Matumaini nk.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook