Your are here: Home // Habari // SANAA BILA WAKONGWE TUNAPOTEA TU- KIPEMBA

SANAA BILA WAKONGWE TUNAPOTEA TU- KIPEMBA

Issa Kipemba

Kipemba mwigizaji wa filamu Swahilihood.

MWIGIZAJI wa filamu na tamthilia Bongo Issa Kipemba almaarufu kama Kipemba amesema kuwa sanaa inahitaji uzoefu na weledi, kulingana na soko lilivyo limefikishwa na ujuaji wa wasanii wa kizazi kipya kilichoteka Bongo Movie na kushindwa kusikiliza wakongwe.

issa kipemba

Kipemba msanii wa filamu Swahilihood

IssaKipemba

Kipemba katika pozi la picha akitokea shamba

“Siku zote wahenga wanasema kuwa Kijiji bila wazee wenye busara ni uwanja wa vita, sasa kama mimi nimejikuta nakaa kimya kushauri hata kutengeneza kazi zenyewe ujuaji mwingi,”alisema Kipemba.

Kipemba anasema kuwa mara nyingi alivyokuwa akipata nafasi na kuongea ukweli kuhusu uaji wa tasnia ya filamu watu walikuwa hawamwelewi lakini kwa sasa ukweli unabainika, kwani anaamini kuwa jamii inahitaji kujifunza kupitia katika filamu na kwa wasanii ambao wanaendana na uhalisia wa maisha yao.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook