Your are here: Home // Habari // FILAMU ZETU ZIVUKA NJE YA MIPAKA TANZANIA– KALEMBO

FILAMU ZETU ZIVUKA NJE YA MIPAKA TANZANIA– KALEMBO

Hashir Khalfan

KALEMBO mwigizaji wa Filamu Swahilihood.

HASHIR Khalfan ‘Kalembo’ mtayarishaji na muigzaji wa filamu ya Sumu amesema kuwa katika utafiti alioufanya katika tasnia ya filamu Bongo kunahitajika kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kwa kutengeneza filamu bora zinashoshirikisha wasanii wa nchi mbalimbali kama filamu yake ya sumu.

Hashir Khalfan

Kalembo akiwa katika moja ya scene katika filamu ya Sumu

Hashiri Khalfan, Salim Ahmed

Kalembo akiwa na mwigizaji mwezake Gabo Zigamba

Hashiri Khalfan

Kalembo akiwa katika pozi la picha

“Naamini soko la ndani tumelishika lakini si rahisi kufika mbali kimataifa bila kuwa na filamu bora na kutoka nje ya mipaka filamu yetu ya Sumu imefungua njia kwa kurekodiwa nchi nyingi,”anasema Kalembo.

Filamu ya Sumu ilizinduliwa katika ukumbi wa sinema wa Century Cinema Mlimani City na kupokelewa kwa furaha kutokana na utofauti uliopo, mtayarishaji huyo pia anasema kuwa sinema hiyo haijatolewa katika Dvd kama ilivyozoeleka bali mashabiki wa filamu waliiona kupitia Azam Tv kwa huduma ya Pay per view.

Filamu ya Sumu imemshirikisha msanii Salim Ahmed ‘Gabo’ Jennifer Temu, Hashir Khalfan ‘Kalembo’ na wasanii wengine kibao, sinema hiyo ilirekodiwa nchini Kenya, Sudan na Tanzania ni kazi ambayo inaonyesha uwekezaji kwa watayarishaji wanaokuja pia kujaribu kubadilisha soko usambazaji kupitia Televisheni badala Dvd

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook