Your are here: Home // Habari // USIKU WA RAMMY NA MASOGANGE UTAKUWA BABKUBWA- RAMMY

USIKU WA RAMMY NA MASOGANGE UTAKUWA BABKUBWA- RAMMY

Rammy Galis

Rammy Galis mwigizaji wa filamu Bongo

MWIGIZAJI wa filamu Bongo Rammy Galis amefunguka kwa kusema kuwa anajipanga kuandaa usiku wa Rammy na Masogange ambao unakuja hivi karibuni huku lengo likiwa ni kuwaonyesha watu jinsi gani alivyoishi na Video Queen huyu ambaye kwa sasa ni marehemu.

Rammy Galis Agnes Masogange

Rammy akiwa na marehemu Masogange enzi za Uhai wake.

Rammy Galis, Duma, Dude, Idriss Sultan

Galis akiwa amebebwa na wasanii wenzake siku ya msiba wa Masogange

Rammy Galis

Rammy katika pozi la picha.

“Nimekuwa nikikimbizana na filamu na tamthilia kwa muda sasa so lakini nataka kuwaonyesha watu kazi yangu na Masogange jinsi nilivyofanya kazi bora inayoitwa Hukumu,”alisema Rammy.

Msanii huyo amesema kuwa baada ya kifo cha mpenzi wake huyo mengi yaliongelewa lakini kupitia filamu yao ya Hukumu majibu yatakuwa wazi na anaamini kuwa itakuwa ndio mwisho wa maswali mengi kutoka kwa watu wengi ambao hawaamini kama Masogange hakuwa msanii wa filamu Bongo Movie.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook