Your are here: Home // Habari // USINGOJE UKWAME PIGA KAZI KWA NGUVU– DAVINA

USINGOJE UKWAME PIGA KAZI KWA NGUVU– DAVINA

Halima Yahaya

Davina mwigizaji wa Filamu Swahilihood.

MSANII wa filamu wa kike Bongo Halima Yahaya ’Davina’ anasema kuwa pamoja na kuigiza kwa msanii anatakiwa kubuni miradi ambayo hata anapokuwa hayupo katika kurekodi lazima anakuwa na kipato cha kuendesha maisha yake na kusubiri hadi akwame mipango yake katika kuigiza.

Halima Yahaya

Davina msanii wa filamu swahilihood

Halima Yahaya

Davina akiwa ameketi katika pozi la picha.

“Sasa kila mtu anatakiwa kuwa mjasiriamali kazi kwenda mbele maisha yanaenda kama hapa mimi nipo na biashara tofauti lakini hapa mgahawani pangu nauza chakula napatikana hapa,”alisema Davina.

Davina anasema kuwa aliamua kufungua Mgahawa TSJ Makumbusho kama ni sehemu yake muhimu anapohitajiwa na wateja wake wa nguo pamoja na biashara nyingine ni rahisi kumfikia japo kuna wateja anaowafikishia bidhaa zake kwa kuwapelekea walipo katika kuvutia wateja.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook