Your are here: Home // Habari // UZINDUZI BONGO MOVIE TASNIA INAKUA AU NDIO KIFO?

UZINDUZI BONGO MOVIE TASNIA INAKUA AU NDIO KIFO?

Mwanaheri Afcery, Flora Mvungi

Wadau wa tasnia ya filamu na wasanii wakiwa aktika moja ya uzinduzi

TASNIA ya filamu kwa sasa ipo katika wakati mgumu sana baada ya watayarishaji wengi kushindwa kuendelea kuzalisha sinema kutokana na kukosekana kwa soko lenye maslahi, takribani miaka 2 sasa hakuna msambazaji wa filamu anayeweza kutoa ofa nzuri kwa ajili ya mtayarishaji.

Ernest Napoleen

Mtayarishaji na mwigizaji wa filamu Ernest katika uzinduzi wa filamu ya Kiumeni

Zero Player film

Filamu ya Zero Player

Chungu cha Tatu film

Filamu ya Chungu cha Tatu

Madebe Lidai

Madebe Lidai mwigizaji anyatamba sokoni kwa sasa.

Mwanahery Afcery

Wadau na wasanii wa filamu wakiwa katika moja ya ukumbi wa filamu kwa ajili ya uzinduzi

Kuna wakati unachanganyikiwa pale unaposikia taarifa kuwa maendeleo ya filamu yanazidi kukua huku sinema nyingi zikiishia katika uzinduzi tu na kuwekwa ndani na kushindwa kuingia sokoni, je uzinduzi huu una tija kwa watayarishaji wa filamu na wadau wake kwa ujumla?

Kwa mfano hivi sasa hakuna tena utengenezaji wa filamu zaidi ya Komedi ambazo nazo ni washiriki ni wale wale, kila komedi ambazo hazina ubora kabisa utaona ni Kipupwe, Mau fundi, Tinny White, Mwanawane na Ringo ndio wanakimbizana na majina ya matukio wakizipa kazi zao.

Sehemu kuu katika kuangalia soko la filamu ni Kariakoo ambapo kwa sasa wale wanaojitaidi kuuza filamu za Kibongo Joh Film, Mbaba Bongo Movie, BMO na Samm Bongo Movie wameamua kurudia filamu za zamani kama Nysuka, Girlfriend, Fungu la kukosa na nyinginezo kwani hakuna filamu mpya.

Filamu hizi za zamani zimejaa ujumbe lakini hazina ubora wa picha na sauti lakini kwa sababu hakuna kazi mpya inabidi wazinunue hizo hizo hali ambayo si salama kwa uendeleaji wa filamu, ni msanii mmoja tu ambaye anatamba na soko na anazidiwa ambaye ni Madebe Lidai pekee.

Maswali yanakuja je wasanii na wadau wa filamu kwa ujumla wake wanawezaje kuendelea na utengenezaji wa filamu mpya na bora? Wengi wanauliza ni kweli kuna vyama au shirikisho ambalo linajaribu kuliangalia hilo au tusubiri uchaguzi tuendelee na nafasi ambazo hazina msaada kwetu?

Nguvu inayotumika kwa sasa kufanya biashara isiyondelevu kwa watayarishaji wa filamu kulipia ukumbi wa kuonyeshea sinema na kugawana kadi huku fashion show zikitawala na kuharibu maana halisi ya Premiere au show ? maswali ni mengi ngoja tusubiri miujiza.
INAENDELEA…

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook