Your are here: Home // Habari // JACK KABIRIGI AMLILIA STEVE NYERERE AMTOE LUPANGO!

JACK KABIRIGI AMLILIA STEVE NYERERE AMTOE LUPANGO!

Jackson kabigiri

Jack Mwigizaji na muongozaji wa filamu Swahilihood.

MUONGOZAJI na mwigizaji wa Filamu Bongo movie Jackson kabirigi ‘Jack’ ameandika barua kutoka mahabusu akiomba msaada wa kutolewa nje baada ya kuwekwa mahabusu kwa kosa la kupoteza vifaa vya studio aliyokabidhi na mmiliki jina lake tunalihifadhi.

Simon Mwakifwamba

Mwakifwamba kiongozi wa filamu Swahilihood.

Steven Mengere

Steve Nyerere mwigizaji

Jackson Kabirigi

Muongozaji wa filamu Swahilihood.

Hata hivyo ombi lake limegonga mwamba baada ya Steve Nyerere kusema kuwa hawezi kuingilia kazi za watu wengine kwani moja ya vyama au shirikisho ni kushughulikia na kusaidia wadau wake ambao ni wasanii hususani filamu hivyo anaona mwenye dhamana hiyo ni Rais wa TAFF Simon Mwakifwamba au uongozi.

“Jamani mimi ni msanii tu wa kawaida pamoja kuwa nina watu wanaoniheshimu na kuniamini, lakini hili la Jack linahitaji msaada kutoka TAFF kama kuna uhalali wa kulifanyia kazi na si mimi,”

“Kama nitafanya hivyo na hizo kamati zao za maafa na mikataba zinafanya nini? Utafanya kwa nia nzuri kesho maneno kila kona steve kaingilia kazi yetu ni vizuri mfuate taratibu sisi tushirikishe tu,”alisema Steve Nyerere.

Baada ya kupata maelezo hayo FC ilimtafuta Rais wa TAFF Simon Mwakifwamba na kuongea naye kuhusu suala hilo ambalo ilionekana kama hajatoa msaada wowote kwa msanii huyo, Mwakifwamba alisema kuwa suala hilo si geni kwani awali alishiriki hadi Jack kupata dhamana.

“Jamani suala hilo chanzo ni mhusika mimi nilikutana na Dr. Cheni na kuongea na Dr. Cheni kumpatia mwanasheria aliyemwekea dhamana, lakini Jack alikimbia na sasa kakamatwa,”alisema Mwakifwamba.

Kufuatia maelezo hayo ni wazi kuwa wasanii na wadau wengine wameombwa kujaribu kumwekea dhamana msanii huyo, lakini Rais TAFF ameshauri kuwa waombwe wasanii wakongwe wajaribu kuongea na mhusika ili suala hilo limalizwe uraiani, kesi ya msanii huyo itasomwa tena tarehe 22 mwezi huu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook