Your are here: Home // Habari // MIMI SI MWANASIASA NAPIGA TAFU TU -WASTARA

MIMI SI MWANASIASA NAPIGA TAFU TU -WASTARA

Wastara Juma

Stara mwigizaji wa filamu

MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Bongo Wastara Juma ‘Stara’ amefunguka kuwa yeye hana mpango wowote kuingia na kugombea cheo kupitia njia ya Siasa kwani hajui ndani ya siasa anaweza kupata nini, lakini anapenda kuwashauri wanasiasa ambao umpa nafasi kuongea nao.

Wastara Juma

Stara mwigizaji wa Filamu Swahilihood.

Wastara Juma

Stara katika pozi la picha

“Mimi si mwanasiasa na sina hakika kama ninaweza kufanya vizuri huko napenda kutumia mitandao ya kijamii kuwashauri wanasiasa ambao ni rafiki zangu pale ninapoona kuna jambo lipo tofauti,”alisema Stara.

“Napenda kuwashauri pale ninapoona kuna jambo linakwenda tofauti naposti na kuongea nao kwa maana wabadilishe lakini si kuingia kwa ndani zaidi,”

Msanii huyo anasema kuna wakati anajikuta anaingia katika malumbano na wale wasiomuelwa wakiamini anapopositi matukio ya kisiasa wakiamini kuwa Stara ana mpango wa kugombea cheo katika chama chake, hivyo anasema yeye ni mjasiriamali na si mwanasiasa ni mshauri tu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook