Your are here: Home // Habari // MARASHI YANGU NI BORA KULIKO!- DAVINA

MARASHI YANGU NI BORA KULIKO!- DAVINA

Halima Yahay

Davina Mugizaji wa filamu Swahilihood

KAMA ilivyo kwa mastaa wengine duniani kuwa na bidhaa zenye majina yao na sasa limeingia kwa wasanii wetu wa filamu ambapo mwanadada Halima Yahaya ‘Davina’ naye anamiliki marashi yake Davina Perfume, mafuta ambayo anasema yamepokelewa vema.

Halima Yahaya

Davina muigizaji wa filamu Swahilihood

Halima Yahaya

Davina muigizaji na mjasiriamali Bongo

“Maisha ni mapambano kila siku kukicha nafikiria jinsi ya kutafuta biashara inayoweza kunisaidia na kutokuwa tegemezi kwa jamii, ukichokwa inakula kwako sitaki kumtegemea mtu,”alisema Davina.

Davina anaamini kuwa yeye kama mjasiriamali anahitaji ubunifu katika kutambulisha bidhaa zake na kuwa bize sana kuwatambua wateja wake kwani kwenye tasnia ya filamu hana hofu uwezo wake wa kuigiza upo juu sana mtayarishaji makini akiwa na filamu lazima amkumbuke.

Davina pamoja na kuuza marashi yak wake lakini pia ni moja kati ya wasanii wajasiriamali wakubwa kwani anamiliki pia mgahawa mkubwa katika baadhi ya Vyuo vyua elimu ya juu sambamba na kuuza nguo, viatu na bidhaa nyingine.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook